Katika mazingira ya Tanzania, ukisikia “mtumishi wa Mungu”, wengi hudhani kwamba ni yule nayefanya kazi ya kutangaza na kuifanya kazi ya kueneza neon la Mungu. Kwa hakika maana hii ni sawa kwa upande Fulani,lakini katika maana halisi ya Kanisa Katoliki, ina maana pana zaidi. Katika kanisa Katoliki,mtumishi wa Mungu (au kwa Kiingereza “Venerable”) ni yule mtu ambae ameshaimaliza kazi yake hapa duniani lakini aliifanya kazi hiyo kiaminifu kwa kuwa ameiishi imani yake kishujaa na sasa Kanisa linaingia katika mchakato wa kuhakiki kama mtumishi yule mwaminifu ameshahesabiwa haki kama ni mtakatifu.
Si jambo la ajabu kwamba maana hii au hatua za utakatifu ni ngeni machoni mwa Watanzania wengi lakini hii inatokana na jambo moja kwamba, katika miaka hamsini ya uhuru, tumekuwa na mtumishi wa Mungu mmoja tu- Mwl. Nyerere, Julius Kambarage na hivyo wengi kuona kama ni ishu ngeni kidogo.
Kuna ngazi kuu tatu ambazo mtu anapitia ili awe mtakatifu, lakini mimi napenda kuziweka nne.
1. Maisha ya uaminifu na ushujaa wa imani.
Mtu anapokuwa anaeuishi ukristu wake kiaminifu anakuwa na nafasi nzuri ya kuishuhudia imani yake kishujaa. Watu wengi watavutiwa na upendo wake kwa Mungu na kwa jirani na kwamba wao wenyewe watakuwa mashuhuda wa kwanza wa matendo ya Mungu kupitia watu hawa mashujaa. Kuuishi ukristu kiaminifu, hauhitaji kufanya miujiza ya kufufua wafu au kuponya wagonjwa, lakini matendo madogo lakini ya upendo mkubwa ni bora zaidi. Hivyo basi, kabla hata taratibu za kikanisa hazijaanza kufatwa, watu wengi watafanya private devotions kwa mashujaa wale.
2. Kutangazwa mtumishi wa Mungu.
Sasa baada ya Kanisa kuona zile private devotions zinavyotia kasi na kwa jinsi ambavyo waumini wanakuzwa imani yao kwa matendo ya Mungu kimwili na kiroho kupitia mtumishi huyu, basi watajibidiisha ili kuchunguza kinachoendelea na wakishajiridhisha, basi wataanza mchakato wa kumtangaza mtakatifu. Hivyo basi watatuma maombi Vatikani na baada ya Vatikani kuridhika basi nao watatoa ruhusa kwamba mchakato uanze napublic devotions ziruhusiwe. Hapo Askofu muhusika wa mahalia atawatangazia waumini na wanachi kwa ujumla akitoa tangazo laitakalotangazwa kwa kipindi cha miezi sita. Tangazo hilo litalenga kuwapa waumini taarifa lakini pia kuwaruhusu kuomba Mungu kupitia maombi ya mtumishi huyo wa Mungu. Atawataka kwamba watakapojibiwa ombi lolote basi wawasiliane na kamati maalumu au kiongozi maalumu wa mchakato huo (postulator).Pia kama kuna mtu anacho kitu chochote cha mtumishi huyo mf. Barua nk. Inabidi pia awasiliane na wahusika aidha kuipeleka nakala halisi au kivuli cha waraka huo.
3. Kutangazwa Mwenyeheri.
Sasa kanisa linahitaji muujiza mmoja ili kumtangaza mtumishi wa Mungu kuwa mtakatifu. Uongo pembeni, hatua hii ni ngumu sana kwani inaweza kuwa ni ya muda mrefu hata karne wa karne. Lakini Mungu huwa na makusudi makuu nay a ajabu sana kwani huwainua watumishi wake pale anapoona ni wakati mwafaka kufanya hivyo kulingana na mahitaji ya kanisa na waumini kwa kipindi kile. Hivyo huwanyanyua watumishi hao kwa malengo tofauti tofauti. Sasa kama ni ugonjwa ndio umepona kutokana na maombi ya mtumishi huyo wa Mungu, basi muujiza huo inabidi uthibitishwe kwamba hakuna science wala nguvu yeyote ya kibinaadamu itakayoweza kuuelezea ubinadamu huo. Hapo itahitaji kuthibitishwa hata na madaktari au wanasayansi ambao hata hawamuamini Mungu. Sasa ile congregation of the doctrine of the cause of saints itamfikishia baba mtakatifu findings zao lakini hata hivyo ni baba mtakatifu pekee ndie mwenye mamlaka baada ya sala kumtangaza mtu kuwa ni mwenye heri.
4. Kutangazwa mtakatifu
Hatua hii ndio kigongo cha vyote kwani mtu anapotangazwa mtakatifu, anakuwa sio tu amenyanyuliwa katika madhabahu ya kanisa lakini pia kitabu cha haki mbinguni. Lakini hii pia ni hatua ngumu sana lakini kila Mungu humpa kila mmoja style ya kipekee.Kwahiyo ukipatikana tena muujiza mwingine basi mwenyeheri basi baba Mtakatifu humtangaza huyo mwenye heri kuwa ni mtakatifu.
Pamoja na ufahamu mdogo wa michakato hii,vilevile huchukua muda mirefu na huwa inakuwa na gharama nyingi lakini kwa uweza wa Mungu hata wale waiotoka katika maeneo duni kabisa, Mungu huwanyanyua katika madhabahu yake kulingana na mapenzi yake.
Tanzania na watakatifu.
Ingawa ninaamini kabisa watakuwepo watanzania wengi tu mbinguni, lakini hakuna ambaye ameshatangazwa hivyo hata sasa. Lakini mapenzi ya Mungu yana nyakati zake na hivyo alimnyanyua Ml. Nyerere miaka ya hivi karibuni kuwa ni mtumishi wa Mungu, na sasa amemnyanyua sista wa kibenediktini kutoka Peramiho.
Kwakuwa mchakato huu umeanza, nitawaletea mfululizo wa matukio mbalimbali kuhusiana na mtakatifu huyu. Hapo ndipo mtakapomjua Sr. Bernadetha Mbawala ni nani na aliishi vipi imani yake Katoliki.
Isubiri sehemu ya pili ya mfululizo huu wa kumuhusu Sr. Bernadetha OSB. Ndani ya upendo wa Kristu, Vicenza-Marie of the Eucharist! | |
daaa kazi nzuri...wengi hatujui hizi ngazi....ila kwa info ulizotupa zitatusaidia sana
ReplyDeleteAsante Dvid, sifa na utukufu kwa Mungu.
ReplyDeletetupo ili tushirikishane.
Deus Meus et Omnia,
Vicenza-marie of the Eucharist
Mungu akubariki kwa kazi njema unayoifanya.
ReplyDeleteKeep up the good work!
SR.Bernadeta Mbawala mtumishi wa Mungu ,amenisaidia katika mengi nitaeleza machache.1.Mimi nilisafiri mpaka Roma/ Itali na baadae Ufaransa Lurdi .Nikiwa Lurdi ,nikiwa napanga nibebe maji matakatifu aliyoagiza Bikira maria tunywe au tuoge wadhaifu wapate nguvu ,wagonjwa wapone.Nilitamani niwabebee masista wagonjwa na wadhaifu wa shirikani yaani alimoishi sr.Bernadetha Mbawala.Kukawa na tangazo hakuna ruhusa kubeba kitu chochote cha majimaji kwenye ndege.Nikakumbuka nimkabidhi Sr.M.Bernadeta Mbawala akafikishe maji hayo.Hivi nilichukua lita ishirini,nikaweka kwenye begi.Siku ya kurudi kufika Roma airport ,begi ile haikuonekana,niliwashirikisha wenzangu na mkuu wetu wa msafara tukaripoti ofisi ,wao wakawasiliana na wanaohusika na mizigo wakasema begi imechanika na hivi tunaifunga vizuri tutaituma.Mara begi ikaonekana imefungwa vizuri na stepula /Plasta ,nilipofungua ndani niliweka picha ya Sr.Bernadeta Mbawala haikulowa pia uzito ulipita wa kawaida tulifanikiwa kupita na kufikisha maji matakatifu ya Lurdi mpaka Tanzania katika shirika la masista Wabenedictini wa mtk.Agnes Chipole na yalitumika kadiri ya lengo.Ilikuwa mwaka 2006 0ctober.Mimi ninaitwa Sr.M.Richardis Chiwinga.
ReplyDeleteSr Richardis asante sana kwa kutushirikisha kwa mwujiza huu. Tuzidi kumuomba Mungu na kushirikishana. Sasa tumepanga kuihuisha blog hii ili tuzidi kuwapa watu taarifa. Tutakamilisha michakato ya TCRA ili tuifanye kwa kufuata sheria za nchi. Asante sana
ReplyDelete