SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Monday, December 5, 2011

Sr. BERNADETA MBAWALA O.S.B - MTUMISHI WA MUNGU - Part 11


Sr. M. Bernadetha Mbawala O.S.B
Ni sista wa jamii ya Masista waafrika WA Mt. Agness  Peramiho, Tanzania, Afrika ya Mashariki. Sr. Bernadeta alizaliwa Peramiho mnamo tarehe 27 Octoba 1911, akafa 29 Novemba 1950.
Wazazi  wakw Stefani na Agata walikuwa ni miongoni mwa Wakristu wa kwanza Peramiho. Katika ubatizo alipewa jina la Klara. Alipokuwa mtoto aliingia shule ya misheni ya Peramiho na alipotimiza umri wa miaka 18 aliingia utawa akaitwa Sr. M. Bernadeta. Akaweka nadhiri zake za kwanza Novemba 11, 1934.
Sr.M Bernadeta alikuwa mgonjwa kwa muda wa miaka 17 akayavumilia maumivu ya kidonda cha stomaki kwa ushujaa. Alijitahidi kijipatia ukamilifu na utakatifu asichoke kamwe. Fadhila zilizojulikana kwake zilikuwa hasa upendo kwa Mungu na kwa jirani, utii, unyenyekevu, uvumuivu, ukweli na usafi mwangavu wa moyo. Akajitoa sadaka kwa moyo mtakatifu wa Yesu kwaajili ya Baba Mtakatifu, mapadre wa dunia nzima ni misioni ya Wabenediktini.
Sasa, mnamo mwezi Juni mwaka 1949, mbali na ugonjwa wa stomaki, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu uliokuwa umefikia hatua mbaya sana. Lakini hata hivyo, hakulegeza bidii ya kuvumilia mateso yote, bali alijibidiisha kuyasetiri huku akiwafurahisha masista wenzie kwa uchangamfu wake. Tokea utoto wake, alimpenda sana Mama Bikira Maria kwa moyo wake laini. Alipokuwa mtoto mwenye mwenye umri wa miaka miwili hivi, alishikwa na ugonjwa mkali wala haikutumainiwa kwamba atapona. Hapo wazazi wake wema walimpeleka kanisani wakamtosa kabisa kwa Bikira Maria Imakulata, akapona.
Muda wa miaka kadha wa kadha kabla ya kifo chake alipata neema za pekee na majaliwa bora nayo yalimsaidia kuyastahimili mateso yake makali kwaajili ya wongofu wa wakosefu na kwa wokovu wa watu walio katika hatari ya kufa.
Kule Peramiho watu waliokuwa na shida kubwa walimlilia Sr. M. Bernadeta kwenye Kaburi lake kwa bidii na matumaini na wengi wao walisema kwamba walisaidiwa kwa maombezi yake.
Basi na tumuombe Mtumishi wa Mungu Sr. M. Bernadeta ili nasi tuweze kumtumikia Mungu kiaminifu.
Pia utakapojaliwa neema yeyote na Mungu mf. Kupona ugonjwa inabidi utoe taarifa ili kusaidia mchakato wa kumtangaza Sr. Bernadeta kuwa Mwenyeheri na baadae kuwa Mtakatifu.

Ndani ya upendo wa Kristu,
Vicenza-Marie of the Eucharist.
Kwa hisani ya Fr. Herbert Meyer O.S.B (Catholic, Mission Liparamba, Mbinga-Songea E.A)

44 comments:

  1. Replies
    1. Nafahamu Sr.bernadetta ni mtumishi wa Mungu nimekuwa nikimuomba mara nyingine na kufanikiwa naomba kupitia kwake muniombee kwani mahusiano na mkuu wangu wa kazi si mazuri hata wafanyakazi wenzangu hawanisemeshi.naomba Mungu aingilie kati kupitia maombezi yake pia
      mke wangu amekuwa mgonjwa kwa miaka mingi akisubuliwa na ukimwi baada ya kuanza novena ya bernadetta mwezi huu ameongezeka uzito toka kilo 50 hadi 55 na hajaungua malaria na hata uso wake unangaa wote wanashangaa.naomba msaaada wenu wa maombezi anaitwa Happiness.

      Delete
    2. Ndugu Anonymous,
      Amani iwe kwako na kwa familia yako!
      Nashukuru kwa kuchangia katika blogu hii lakini cha mno ni kushukuru kwaajili ya nia yako njema ya sala za Sr Bernadetha Mbawala na sie nduguzo katika Kristu.

      Nitaweka sala ambayo jimbo kuu la Songea imeitoa maalumu kwaajili ya Sr. Bernadetha na kuomba watu watoe shuhuda zao pia.
      Kwa zaidi,Ungeweza kupata mchanga wa kwa kaburi la sista ungemchanganyia Happiness. Mungu anaweza kumtumia mkeo ili kumtakatifuza Sr Bernadetha katika madhabahu yake basi tuungane katika sala.

      Kuhusu kazini nakusihi uvumilie kwa saburi ukimchukulia kila mmoja kwa upendo.Katika Matayo 5:44 Yesu anasema tuwapende maadui zetu (Wale wanaotuchukia) basi tujifunze kutoka katika Mtakatifu Teresa wa mtoto Yesu tukivumilia na kuwatolea tabasamu wale wote wanaotuchukia tukiutolea moyo Mtakatifu wa Yesu.

      Basi tuzidi kutiana nguvu.

      Katika Kristu,

      Vicenza-marie of the Eucharist!

      Delete
    3. Sawa,kwa ushauri nigetamani kupata mchanga kwani hali yake inaendelea vizuri.Nadhani nitafuga safari kuja huko songea kwani niko mkoa wa Mara.Nadhani si vigumu kuupata mchanga.
      martin zacharia

      Delete
    4. Kama haujapata mchanga tuwasiliane kwa 0755466982

      Delete
    5. Nami nasumbuliwa na uzazi na maelewano mabovu kazini nisaidieni mchanga

      Delete
  2. Veberable Sr. Bernadeta Mbawala O.S.B, Ora pronobis

    ReplyDelete
  3. tunashukuru...nadhani naomba uniruhusu niicopy ili nikawaeleze wakatoliki wenzangu hapa chuoni ili kupitia mtumishi wa Mungu huyu watu waombe na tuweze kufanikisha mchakato,...ila niliuliza lini ametangazwa kuwa mtumishi wa Mungu na misa ya kuanzishwa kwa mchakato wake ilifanyikia wapi,...na kanisa mahalia wamejipangaje kuusimamia huu mchakato..maana naona mchakato wa mwalimu ni kama vile umepoa...am scared

    ReplyDelete
  4. Mchakato ulitangazwa Rasmi kanisani tarehe 13 Novemba, 2011 Jimbo Kuu la Songea. Umeanza kwa kasi ya ajabu usipime.

    Vicenza-Marie of the Eucharist!

    ReplyDelete
  5. Watu wengi wanaomba sala iliyotolewa rasmi ya maombezi tafadhali ichapishe hapa.Ili wamuombe Mtumishi wa Mungu.Nakumbuka ya Mwalimu Nyerere ilitolewa.Tafadhali saidia hilo

    Zacharia Martin
    5/03/2012

    ReplyDelete
  6. nimewahi kufika katika kaburi lake zamani sana labda 1990.nikachukua udongo wa kaburi lake nikielekezwa na rafiki zangu.nilikuwa mdogo sana wakati huo.niliporudi nao,akaniomba dada mmoja aliyekuwa mgonjwa wakati huo.nikampa na baada ya siku moja baadaye akafariki dunia.ni moja ya matendo makuu niliyowahi kufanya duniani.tangu wakati huo hadi leo sijafika tena Peramiho.ila nina imani kubwa na sr.Benadeta OSB..Hivi kinaendelea nini,nasikia kuna jopo la watu lilikuja kufanya uchunguzi,je mwili wake bado upo pale?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli ukipitia posts mbalimbali utapata ufahamu zaidi na sasa nimepata information nyingi mno basi nitaanza kuziposti baada ya kuirekebisha hii blogu.

      Sifa na utukufu kwa Mungu Mbinguni


      Vicenza-Marie!

      Delete
  7. naomba kujua ni nani alikuwa wakwanza au ilikuwaje mpaka, watu wakona kugundua upekee wa sr. benedette, kwa ujumla nataka kujua historia yake kwa undani.

    ReplyDelete
  8. Maisha yake kwa ujumla yalikuwa ji ya kipekee mno na pengine ikawa ngumu kuhakiki nani hasa alikuwa wa kwanza kwa sababu inawezakuwa masista wenzie lakini kama hawakutoa taarifa ni vigumu kuthibitisha hilo lakini taarifa rasmi na ambazo ni sahii, mtu wa kwanza kugundua alikuwa ni baba yake mshauri wa Kiroho padre mswiss ambaye amekiandika hiki kijitabu cha maisha ya Sr. Bernadetha na ni huyu padre baada ya kugundua upekee wa maisha ya Sr. Bernadetha, alimwambia aandike kuhusu maisha yake na ndiyo matokeo ya vitabu vingine nane ambavyo bado kutolewa hadharani ingawa vimeshapitiwa na wanateolojia kwa ngazi ya jimbo mahalia yaani jimbo kuu la Songea


    Vicenza
    -Marie

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kweli Sr.Bernadetha anastahili kutangazwa Mtakatifu, nimekuwa nikimwomba kila mara tangu enzi za chama cha kipapa Pale peramiho. Nimeshuhudia watu wa kila aina wakienda kusali kwenye kaburi lake hasa watoto, wagonjwa na wanafunzi. sisi tuliosoma Peramiho Girls tunaweza kusimulia hili. mimi na mama yangu daima tunamkimbilia Sr. Brnadetha Mbawala tukiwa na shida na tunasaidiwa.

      Furaha Kapinga

      Delete
  9. Mimi naomba mama benadeta mbawala aniombee sababu shida yangu ni mtoto katika ndo yangu ili niweze kuwa na furaha ya amani katika maisha yangu ya ndoa.

    ReplyDelete
  10. Mimi naomba mama benadeta mbawala aniombee sababu shida yangu ni mtoto katika ndo yangu ili niweze kuwa na furaha ya amani katika maisha yangu ya ndoa.

    ReplyDelete
  11. Tyk. Naomba kupata hiyo sala maalum ya mtumishi Sr Mbawala

    ReplyDelete
  12. Nashukuru, nilipata udongo wa kaburi lake, nmekua nikihangaika katika masomo kwa muda mredu na nimefanikiwa mwaka huu

    ReplyDelete
  13. Nimewapa udongo wa kaburi la Bernadeta Mbawala wagonjwa wa wili walikuwa wamehangaika sana na ugonjwa wa pumu na mwingine ugonjwa wa kuanguka yaani kifafa wote wamesema wamepona ,hawapati tena shida hiyo .majina nitayataja baadaye.Ninamshukuru Mungu pamoja nao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana kwa mrejesho. Mungu awabariki sana

      Delete
  14. TYK. nimepata habari za Mtumishi wa Mungu Sista Bernadeta Mbawala kupitia Kitabu cha Nguvu ya Sala cha Angela Benwdict Kessy. Naomba kutumiwa udongo wa kabuti lake, nipo Arusha. Pia naomba hiyo sala ya kuomba kupitia Sista Bernadeta Mbawala

    ReplyDelete
  15. Natamani sana kupata udongo Wa huyu sista.Ulinisaidia sana kipindi nasoma huko.

    ReplyDelete
  16. Naomba kujua taratibu za kupata huo udongo wa Sister B,

    ReplyDelete
  17. Hello ndugu.I want to know now sr.bernadeta mbalawa is servant of god or venerable.also may I have to contact to postulator of this cause .my WhatsApp number is +255628969533.

    ReplyDelete
  18. Hi. She's still the Servant of God. Her cause was officially closed at the national level...waiting for Vatican processes then, God willing, she will be a Venerable. Your WhatsApp number is noted.

    ReplyDelete
  19. Mungu baba atulngoze katika mchakato mzima huu

    ReplyDelete
  20. Naomba kutumiwa sala ya kumuomba sr.Benadetha mbawala jamani.

    ReplyDelete
  21. Namshukuru mungu nimepata Sala ya Mtumishi wa Mungu, Sr. Bernadetha Mbawala, hakika ndani ya siku chache nimeyaona matunda mazuri sana. Maana nilikuwa na shida nyingi sana lakini zote nilipoomba kupitia yeye kila shida naona mafanikio makubwa sana. Asante mke wangu Salome nothickery mwenda kwa kuniunganisha na mtumishi huyu. Baada ya kufanikiwa rasmi nitaandika barua rasmi ya ushuhuda ili mchakato wake wa kuwa mwenye Heri ufanikiwe haraka na kisha Mtakatifu. Naitwa Augustino Alex Ngailo, kutoka mkoa wa Njombe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba pia nakala ya Sara yake na namna ya kupata mchanga wake

      Delete
  22. Na mimi nina shida na kupata Mchanga wa kaburi lake, namba yangu ya simu: 0766178770 au 0655178770

    ReplyDelete
  23. Naomba kutumiwa Sala maalumu ya kimuomba Mt bernadeta,0765165670

    ReplyDelete
  24. Naomba kutumiwa Sala ya Sr Benadeta mbawala .0786186156 Agnes luambano

    ReplyDelete
  25. Naombeni sala au kama ana novena huyu mtakatifu nimetafuta parokia nyingi nimekosa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tumsifu Yesu Kristu!
      Naomba kupata maelekezo namna ya kuutumia huo udongo

      Delete
  26. Tumsifu Yesu Kristu
    Naomba kupata maelekezo namna ya kuutumia huo udongo

    ReplyDelete
  27. Tumsifu Yesu Kristo wapendwa, ni kwa mda sana nimekua nikiomba kwa maombezi ya Sister Benerdetha Mbawala, nimepata shuhuda nyingi sana kwa kupitia maombezi yake.
    1. Mama yangu alikua amepata dalili za kisukari, tuliofu sana ila nilioosali sala ya Mtumishi wa Mungu Sr B.Mbawala mama yangu alipona kabisa sukari na mpaka sasa yapita miaka minne tangia apone na wala dawa atumii kabisa.
    2. Kulikua na rafiki wa familia yetu alikua anaitwa Benadetha pia, aliugua sana na kulazwa ICU kwa mda mrefu bila matumaini, ila kuna siku tulimtumia sala hii ndugu wa karibu wakaanza kusali kwa imani Benadetha alitoka ICU na akaendelea kuomba mwenyewe mpaka alivyoruhusiwa kutoka hospitalini.
    3. Baba yangu alipata vidonda vya tumbo vilivompelekea kutapika damu nyingi sana, tulisali sala hii ya Sr Benadetha na mpaka leo hasumbuliwi tena.
    4. Mimi binafsi nikiwa naumwa kila nisalipo Sala hii hua napona mara moja.

    Sala ya Sr Benadertha nayoitumia iko kwenye kitabu cha nguvu ya Sala.
    Asante 🙏🏼

    ReplyDelete
  28. Habari tafadhali ninaomba kupata Nakala ya salaam ya Sr Benadetha,, tayari nlikwenda juzi kupata udongo katika kaburi lake naomba kuipata Sala ili inisaidie kuomba.
    NOTE; Ni muhimu Sana
    Ni 0679158309
    Devis Nchimbi. Songea

    ReplyDelete
  29. Kristu namshuru Mungu kupitia sala hii ya sir. Mbawala na Mimi naomba mchanga wa Kabuli lake kama Bado unapatikana nipo sengerema Mwanza 0621650169

    ReplyDelete
  30. Mimi nipo peramiho na sijawahi kusikia habari hizi nzuri jaman,pengineni wakati sahihi Sasa Mungu ametaka nizijue habar hz,kwa aliyepo peramiho naomba tuungane pamoja tutafte mwenyeji atupeleke pamoja kwenye kabur la huyu mtakatfu tukapate mchanga wake na tupate fursa ya kusali hapo..namba zangu ni 0768946088🙏

    ReplyDelete
  31. Mimi Evodius Kamugisha, Tunaomba Sala ya Maombezi ya Mtumishi wa Mungu, Sr Bernadetha Mbawala.
    Iwekwe kwenye hii blog ili waumini wapate kutumia kuomba msaada wa maombezi

    ReplyDelete
  32. Mimi nimefanikiwa kufika hapo Peramiho, ndo nilipewa hii habari njema ,ambayo nilikuwa sifaham.
    Tunaomba juhudi kupitia Radio Maria , Tumaini Tv, Tumaini Radio, Jugo media, Matendo makuu ya Mwenyezi Mungu yatangwe kwa nguvu zote.

    ReplyDelete

Dear Rafiki,
Asante kwa comments zako


Vicenza-Marie!