SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND
Showing posts with label Maisha ya Sr. Bernadeta. Show all posts
Showing posts with label Maisha ya Sr. Bernadeta. Show all posts

Monday, May 28, 2012

KITABU KUHUSU MAISHA YA SR. BERNADETA SASA KINAPATIKANA DAR

Kristo!

Wengi walikuwa kiulizia upatikanaji wa kitabu kuhusu maisha ya Sr. Bernadeta Mbawala. Napenda kuwajulisha kwamba kitabu hiko sasa kinapatikana hapa Dar. Acha email yako hapa kwenye comments kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kukipata.
Sr. Bernadeta Mbawala mwandishi ni Pd. Heribert Meyer

MTOTO ALIYEPATIKANA MWA MAOMBEZI YA SR. BERNADETA MBAWALA

Kristu!

Amani na salama kwenu!.

Ingawa wapo watu ambao wameanza kumfahamu Sr Bernadeta hivi karibuni, ukweli ni kwamba Sr. Bermadeta alianza kufahamika hata kabla hajafariki akiwa ni Sr. mgonjwa tena ambaye si msomi. Utakatifu wa Sr. huyu mnyenyekevu ulionekana toka siku hizo. Hii nitaeleza katika maandihi yajayo nikimnukuu Pd. Meyer ambae amemuandika sana Sr. Bernadeta Mbawala.

Sasa baada ya kifo chake, waumini wengi walimiminika katika kaburi la Sr.m Bernadeta wakiomba maombezi yake kwa Mungu. Ni mengi yamesimuliwa, shuhuda nyingi tamutamu zimetolewa na sasa miujiza mingi zaidi inazidi kutendeka katika kaburi hilo.

Sr.Veronika Tiamalis aliyepatikana kwa maombezi ya Sr. Bernadeta akiwa na mama yake
Leo tuangalie shuhuda ya Mama Veronika ambae hakuweza kupata mtoto na hivyo alimkimbnilia Sr. Bernadeta amuombee ili apate mtoto. Basi mama huyu alisikiwa na Mungu akamjalia mtoto kwa kupitia maombezi ya Sr. Bernadeta. Naye mtoto huyo si mweingine bali ni Sr. Veronika Timalias wa shirika la wabenediktini wa Tutzing Pramiho - Songea.

Nawahimiza wasomaji wote kumkimbilia Sr. Bernadeta katika shida zenu mbalimbali na hasa nawahimiza wanawake wenye matatizo ya uzazi.

Iwapo Mungu atakujalia neema yeyote kupitia maombezi ya Sr Bernadeta basi usisite kutoa taarifa.

Wednesday, April 18, 2012

KITABU KUHUSU MAISHA YA Sr.BERNADETA MBAWALA

Dear Marafiki,
Nimekikuta hiki kitabu online sijajua kama lugha ni kijerumani au la. Nitawasiliana na kamati ya mchakato Jimbo ili nijue kama ni kimoja ya vitabu vilivyoletwa kutoka Ujerumani aub la.

Tsa bophelo ba Sister M. Bernadetta Mbawala, O.S.B., oa kopano ea masistere a ma-Afrika a Agnes ea Halalelang, a Peramiho, Tanganyika, 1911-1950

 

 

Bibliographic information

QR code for Tsa bophelo ba Sister M. Bernadetta Mbawala, O.S.B., 
oa kopano ea masistere a ma-Afrika a Agnes ea Halalelang, a Peramiho, 
Tanganyika, 1911-1950