SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Wednesday, December 21, 2011

MFAHAMU MT. FRANCIS WA SALES


Maelezo mafupi kuhusiana na mtakatifu Francis wa Sales.
Baba yake na Francis alidhamiria kumuona mwanae anakuwa hakimu na hivyo akampeleka shule mapema. Akiwa huko alisoma maswala ya lugha na  maswala ya jamii chini ya usimamizi wa Wajezuiti.Akiwa hapo alianza pia kozi ya teolojia HAPA SASA SOMA KWA MAKINI.
 Sasa kulikuwa na mijadala mikala sana ya wanateolojia kipindi hicho kkkutoka dini na madhehebu mbalimbali kuhusiana na maswala ya imani na hasa maswala ya predestination(kwamba kama mambo yote amabyo yanatokea ni mapenzi ya Mungu na mungu ameshayapanga. Mf. Kama Mungu amekupangia uende motoni basi hata ufanye nini wewe ni wa motoni) Haya ndiyo yalikuwa baadhi ya mabishano. Mengine ni kama kuhusu Bikira Maria, Ekaristi, wokovu na mambo mengine ambayo humu tunaelekezana. Sasa Mt. Francis aliogopa na kutishika sana hata akaelekea kupoteza tumaini kabisa lakini siku moja ghafla alifunguliwa alipopiga magoti katika sanamu ya miujiza ya Bikira Maria wa Mt. Etienne wa Greez. Basi toka siku hiyo akaweka nadhiri ya usafi wa moyo na kujitoka kabisa kwa mama Bikira Maria.
Sasa ilipotokea reformation ya waprotestant  alihubiri sana injili  kwa utakatifu wake, upole na ushujaa. Akajitolea kuinjilisha maeneo mbalimbali ikiwemo Geneva Aliyahatarisha sana maisha yake katika kipindi kile kigumu Aliwashinda wahubiri wakiprotestant waliotumwa kwenda kubishana nae na theologians wengi wa kiprotestant wakabadili dini na kurudi ukatoliki. 

Thursday, December 8, 2011

JE BIKIRA MARIA NI NANI? KWANINI WAKATOLIKI WANAMPA KIPAUMBELE SANA?


Dear Rafiki
Tukiwa tunasherehekea sikukuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, na miaka 47 ya nchi ya Tanzania kuwekwa chini ya ulinzi wa Mama Maria Imakulata, nawaletea juzuu hii ili wale wasiomfahamu wapate kumfahamu, wale waliomsahau wapate kumkumbuka na wale wanaona shaka wapate kuelewa. Karibu!

MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA B. MARIA


Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya imani yao ama wenyewe  wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu, tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu wote pamoja na Yohane Mbatizaji, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27). Hivyo yale yote tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia  kwa hiari fumbo la mpango wake.
MAANDIKO YANASHUHUDIA UMUHIMU WA WATU UNAOTOFAUTIANA
 Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake. Abrahamu alimuamini na kuwa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18). Yosefu, kipenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20). Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale:
aliongoza Israeli kutoka utumwani Misri akalipatia  sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, “Wala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12). Kwa kuwa watu hao ni wengi mno tunaorodhesha wafuatao: Yoshua, Debora, Gideoni, Samsoni, Samweli, Ruthu, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Yeremia na Ezekieli. Nabii Isaya ana sifa ya pekee katika kumchora Masiya. Mwishoni Bwana Yesu mwenyewe anamsifu Yohane Mbatizaji akisema, “Ni mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).
Bikira Maria ana nafasi gani kati yao? Hao tuliowataja walitenda kweli mambo makuu kwa imani, lakini Bikira Maria yuko juu sana kupita hao wote, tena kwa mbali: yeye ni malkia wa makundi yote ya mbinguni, sio ya watutu, bali hata ya malaika. Mapokeo ya mashariki humuita “daraja linalounganisha dunia na mbingu”, “mfano aliouona Yakobo” (Mwa 28:12).

BIKIRA MARIA KATIKA BIBLIA

UTABIRI KUHUSU BIKIRA MARIA, EVA MPYA Mapokeo yamtazama Bikira Maria kama Eva mpya atakayemshinda nyoka wa kale (Ibilisi). Kwa nini Eva mpya? Kwa sababu Eva wa kale alidanganywa na kuangushwa na Shetani, hivyo alitenda dhambi. Kumbe Maandiko matakatifu yanatupatia utabiri kuhusu Eva mpya atakayemshinda adui (Shetani) kwa kumponda kichwa: “Nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15).
“Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo lilinganishwe  na Lk 1:34-35, “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu  zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”. Utabiri mwingine wasema, “Litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho ya hekima na ufahamu, Roho wa shauri na uwezo, Roho wa maarifa na ya kumcha Bwana” (Isa 11:1-2). Je, shina hilo si yeye Mama Bikira Maria, na tawi alilochipusha si Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo?
 “Umebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9). Linganisha dondoo hili na Lk 1:42, “Akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa”. Je, utasema Bikira Maria ni mtu wa ziada katika mpango wa Mungu? 
Tena tunasoma, “Imba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu  katikati yako” (Sef 3:14-15). Linganisha dondoo hilo na Injili: “Malaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja nawe” (Lk 1:28).

BIKIRA MARIA KATIKA AGANO JIPYA
Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yametimia katika Agano Jipya: ukombozi wetu ulianza pale Bikira Maria alipokubali fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu, akisema kwa hiari, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38). Je, Bikira Maria ni bahasha? Siku hizi kuna baadhi ya waheshimiwa ambao wanadhani kujua Maandiko kuliko watu wengine, tena wanadai wanaye Roho Makatifu; kumbe wanadiriki kumuita Mama huyo mtakatifu, eti ni “bahasha” ambayo ikileta barua haina kazi! Jambo hili linasikitisha sana na sio tu kumkosea heshima Mama yetu mpendwa wa mbinguni, bali inaweza pia kuwa kufuru kwa Mwenyezi Mungu aliyemuumba kama msaidizi wa Mkombozi aliyejaa neema. Manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua kwa heshima; Mama Elizabeti alijiona hastahili kutembelewa naye akamuita, “Mama wa Bwana wangu”; mzee Simeoni alimuagulia mateso yenye uchungu kama upanga yatakayopenya moyowe. Bwana Yesu aliyefurika Roho Mtakatifu tangu nukta ya kuchukuliwa mimba, wakati alipokaribia kufa pale msalabani alimuita, “Mama”; jumuia ya Mitume na wafuasi wa kwanza walimtaja kipekee ilivyo ishara ya heshima. Je, Roho Mtakatifu ndiye anayewaongoza hawa ndugu zetu wamuite bahasha? Je, ni Roho yuleyule aliyewaongoza Mitume na manabii ama roho ya aina nyingine? “Wapenzi wangu, msisadiki kila mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni” (1Yoh 4:1).
Bikira Maria sio “chombo” tu, bali mshiriki wa kazi ya ukombozi ya Mwanae. Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, “Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol 1:24). “... maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b). Katika hilo la kumfuata Mwanae katika mateso Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni, “Tazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiteswe na Herode, “Hivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufa” (Math 2:14-15).

BIKIRA MARIA MWOMBEZI KATIKA HARUSI YA KANA:  Mama Bikira Maria anaonekana mwenye kuonea huruma wenye shida: kwa ombi lake huko Kana ya Galilaya Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini (Yoh 2:1-12).

BIKIRA MARIA AFANYWA EVA MPYA:  Juu ya Eva wa zamani imesemwa ni Mama wa walio hai: “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Agano Jipya linaonyesha Adamu na Eva wa zamani wametuletea kifo (Rom 5:12).
Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Bikira Maria awe Eva mpya kwa kitendo cha kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. “Basi Yesu aipomwona Mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda amesiMama  karibu akamwambia Mama yake, Mama, tazama Mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama Mama yako” (Yoh 19:26-27). Zaburi yasema, “Lakini juu ya Sion itasemwa, Sion ni Mama yao wote; Mungu mkuu ameuthibitisha. Mwenyezi Mungu ataorodhesha mataifa na kuandika juu ya kila moja, Huyu chanzo chake ni Sion” (Zab 87:5-6). Pale msalabani Bikira Maria:
        alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae;
        alifanywa malkia wa wafiadini;
        kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa;
         katika kuteswa kwa Yesu Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua; wanafunzi wa Yesu walipokimbia na kumtazama kwa mbali, Bikira mtakatifu alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata. Tena kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, aliposhuhudia mateso ya Mwanae aliteseka sana katika moyo wake safi usio na doa, kiasi kwamba baadhi ya watakatifu wanasema, Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote, Yesu mwilini na Mama yake moyoni. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo. 

JE, BIKIRA MARIA ALIZAA WATOTO WENGINE?
 Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Alikufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni “Bikira daima”.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani? Wanaosemwa katika Injili “ndugu zake Yesu” si watoto wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, “‘Mwana, tazama Mama yako’. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yoh 19:27). Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo “ndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na mama yao kwenye Injili anaitwa “Maria mwingine”, si Maria Mama wa Yesu. “Walikuwepo pia wanawake waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo na Yose” (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama “Mama wa Yesu”.
 JE, WAKATI WA KUFANYA UTUME YESU ALIMDHARAU MAMA YAKE?
 Wengine husoma Maandiko matakatifu wakiishia ujuu bila ya kufikiria wala kulinganisha na mistari mingine. Hivyo hukwazwa na semi kadhaa za Bwana Yesu ambazo  kimsingi hazimpingi Mama yake, bali zinampongeza. “Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akasema, ‘Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, ‘Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishika’” (Mk 11:27-28).
Tena lingine lasema, “Basi, mtu mmoja akamwambia, ‘Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, ‘Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’ Kisha akanyosha mkono wake juu y aweanafunzi wake akasema, ‘Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na Mama yangu’” (Math 12:46-50).
Je, sehemu hizi za Maandiko zinampinga kweli Bikira Maria au zinampongeza? Sababu:
        Jamaa yake Elizabeti alimpongeza, tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, “Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).
        Bikira mtakatifu alipopashwa habari na malaika hakukataa mpango wa Mungu, bali kwa hiari yake alikubali fumbo la mpango wake. “Maria akasema, ‘Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena’. Kisha malaika yule akaenda zake” (Lk 1:38).
        Bwana Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya Kiroho kuliko ya mwilini. Hivyo ni kweli, Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake, iliyokuwa ya juu zaidi kushinda hata ile ya Abrahamu, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Hata hivyo tusisahau kuwa Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu wazazi wake, tena tunasikia aliwatii. “Basi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatii” (Lk 2:51).
Naomba, kabla hujahukumu neno moja, angalia ujumla wake.
Yesu alizaliwa na Bikira mtakatifu, ndiye aliyemlea na kuhangaika naye huko na huko hata Misri ili kumuepusha na kifo. Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara iliyongozwa na Bikira Maria huko Kana. Maria alikuwepo hata wakati wa Yesu kuteswa, akiteseka pamoja naye. Pale msalabani alikabidhiwa Kanisa kwa njia ya Yohane mtume. Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, na ndiye aliyelivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa njia ya sala yake. “Hao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zake” (Mdo 1:14).

DOGMA ZA KANISA KUHUSU BIKIRA MARIA
 Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na ufunuo wa Mungu:
1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili
2. B. Maria Mama wa Mungu 
3. B. Maria Bikira daima
4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho
MKINGIWA DHAMBI YA ASILI
Tunasadiki Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye mwanakanisa aliyekombolewa kwa namna bora kushinda viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita APanagia = Mtakatifu tu. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, hata mwaka 1858 Bikira Maria alijitambulisha huko Lurdi (Ufaransa) kwa Mt. Bernadetta Soubirous kama Mkingiwa. Tena pale Fatima (Ureno) tumefunuliwa moyo wake safi usio na doa.
MAMA WA MUNGU
  Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana ndiye aliyetwaa ubinadamu katika Bikira Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi isipokuwa hana dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu, hivyo akisema, ‘Mimi’, anamaanisha Nafsi yake ya Kimungu. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, “Kweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepo” (Yoh 8:50). “Kama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yoh 5:26). Je, Bikira Maria ni Mama wa Mungu tangu lini? Mtume Paulo anaeleza, “Wakati maalumu ulipotimia Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4). Ni kwanzia wakati huo: sasa imepita miaka 2006 tangu Bikira Maria ajiliwe na sifa hiyo ya kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika, akawa malkia wao. “Malaika alimwambia, ‘Hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu’” (Lk 1:35). Dogma ilitolewa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa Efeso uliomuita “Mzazi wa Mungu”.

BIKIRA NA MAMA
 Fumbo la Bikira Maria hapa linagongana na akili ya kibinadamu. Wote wanakiri ya kuwa Yesu alimwilishwa bila ya mchango wa mwanamume, kumbe la ajabu zaidi ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali uliutakasa. Ingawa akili yetu inakataa, sisi tunakiri na malaika, “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1:38). Ndiyo maana tunamkiri ni Bikira daima.

KUPALIZWA MBINGUNI MWII NA ROHO
 Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria mwenye heri alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya mwanamke mshindi. “Ishara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake” (Ufu 12:1).

HESHIMA ZA LITURUJIA KWA MARIA
Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia. Hapa tunazipanga kulingana na heshima zinavyozidiana:

SHEREHE
8 Desemba – Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili
1 Januari – Bikira Maria Mama wa Mungu
25 Machi – Bikira Maria Kupashwa Habari
15 Agosti – Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni
SIKUKUU
31 Mei – Maamkio ya Bikira Maria
8 Septemba – Kuzaliwa kwa Bikira Maria

KUMBUKUMBU
Juni – Moyo Safi wa Maria
15 Septemba – Mama Yetu wa Huzuni
22 Agosti – Bikira Maria Malkia
7 Oktoba – Bikira Maria wa Rozari
21 Novemba – Bikira Maria Kutolewa Hekaluni

KUMBUKUMBU YA HIARI
11 Februari – Mama Yetu wa Lurdi
16 Julai – Mama Yetu wa Mlima Karmeli
5 Agosti – Kutabaruku wa Kanisa la B. Maria 
 Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu. Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria mwenye heri: mashariki tenzi na nyimbo (k.mf. Akatistos, tenzi za mt. Efrem shemasi, na nyingine); magharibi (Roma) tunamheshimu binafsi na hata kijumuia kwa kusali rozari takatifu. Ndiyo ibada ya binafsi inayompendeza sana baada ya zile za liturujia hata akatokea sehemu mbalimbali duniani akihimiza tusali rozari ili tupate amani binafsi, kitaifa na kimataifa.
 Mwezi wa tano ni mwezi wa Maria. Mwezi wa kumi ni mwezi wa Rozari. Mtu aliyeonja matunda ya kumheshimu Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, anajua uwezo wa maombezi yake. Kanisa linakiri neema zote za Mungu zaja kwetu kwa njia ya Maria.Je, tunamuabudu Bikira Maria? Hapana, Bikira Maria hatumuabudu hata kidogo, bali tunamtolea heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Mungu tu tunampa heshima ya ‘latria’ (kuabudu), watakatifu tunawaheshimu (dulia) na Bikira Maria tunampa heshima sana (yuper-dulia). Kweli Mama Bikira Maria ni “kina kisichochungumzika kwa macho ya malaika” (Akatistos).
 Ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Katika Injili ya Yohane Bwana Yesu alisema, “Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa. Tena katika Injili ya Luka kuna utabiri wa kumheshimu Bikira Maria vizazi vyote, “Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote
wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).
 Una la nyongeza? Twangaaaaa
  

Monday, December 5, 2011

Sr. BERNADETA MBAWALA O.S.B - MTUMISHI WA MUNGU - Part 11


Sr. M. Bernadetha Mbawala O.S.B
Ni sista wa jamii ya Masista waafrika WA Mt. Agness  Peramiho, Tanzania, Afrika ya Mashariki. Sr. Bernadeta alizaliwa Peramiho mnamo tarehe 27 Octoba 1911, akafa 29 Novemba 1950.
Wazazi  wakw Stefani na Agata walikuwa ni miongoni mwa Wakristu wa kwanza Peramiho. Katika ubatizo alipewa jina la Klara. Alipokuwa mtoto aliingia shule ya misheni ya Peramiho na alipotimiza umri wa miaka 18 aliingia utawa akaitwa Sr. M. Bernadeta. Akaweka nadhiri zake za kwanza Novemba 11, 1934.
Sr.M Bernadeta alikuwa mgonjwa kwa muda wa miaka 17 akayavumilia maumivu ya kidonda cha stomaki kwa ushujaa. Alijitahidi kijipatia ukamilifu na utakatifu asichoke kamwe. Fadhila zilizojulikana kwake zilikuwa hasa upendo kwa Mungu na kwa jirani, utii, unyenyekevu, uvumuivu, ukweli na usafi mwangavu wa moyo. Akajitoa sadaka kwa moyo mtakatifu wa Yesu kwaajili ya Baba Mtakatifu, mapadre wa dunia nzima ni misioni ya Wabenediktini.
Sasa, mnamo mwezi Juni mwaka 1949, mbali na ugonjwa wa stomaki, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu uliokuwa umefikia hatua mbaya sana. Lakini hata hivyo, hakulegeza bidii ya kuvumilia mateso yote, bali alijibidiisha kuyasetiri huku akiwafurahisha masista wenzie kwa uchangamfu wake. Tokea utoto wake, alimpenda sana Mama Bikira Maria kwa moyo wake laini. Alipokuwa mtoto mwenye mwenye umri wa miaka miwili hivi, alishikwa na ugonjwa mkali wala haikutumainiwa kwamba atapona. Hapo wazazi wake wema walimpeleka kanisani wakamtosa kabisa kwa Bikira Maria Imakulata, akapona.
Muda wa miaka kadha wa kadha kabla ya kifo chake alipata neema za pekee na majaliwa bora nayo yalimsaidia kuyastahimili mateso yake makali kwaajili ya wongofu wa wakosefu na kwa wokovu wa watu walio katika hatari ya kufa.
Kule Peramiho watu waliokuwa na shida kubwa walimlilia Sr. M. Bernadeta kwenye Kaburi lake kwa bidii na matumaini na wengi wao walisema kwamba walisaidiwa kwa maombezi yake.
Basi na tumuombe Mtumishi wa Mungu Sr. M. Bernadeta ili nasi tuweze kumtumikia Mungu kiaminifu.
Pia utakapojaliwa neema yeyote na Mungu mf. Kupona ugonjwa inabidi utoe taarifa ili kusaidia mchakato wa kumtangaza Sr. Bernadeta kuwa Mwenyeheri na baadae kuwa Mtakatifu.

Ndani ya upendo wa Kristu,
Vicenza-Marie of the Eucharist.
Kwa hisani ya Fr. Herbert Meyer O.S.B (Catholic, Mission Liparamba, Mbinga-Songea E.A)

Thursday, December 1, 2011

SR. BERNADETHA MBAWALA OSB -MTUMISHI WA MUNGU- Part 1



Katika mazingira ya Tanzania, ukisikia “mtumishi wa Mungu”, wengi hudhani kwamba ni yule nayefanya kazi ya kutangaza na kuifanya kazi ya kueneza neon la Mungu. Kwa hakika maana hii ni sawa kwa upande Fulani,lakini katika maana halisi ya Kanisa Katoliki, ina maana pana zaidi. Katika kanisa Katoliki,mtumishi wa Mungu (au kwa Kiingereza “Venerable”) ni yule mtu ambae ameshaimaliza kazi yake hapa duniani lakini aliifanya kazi hiyo kiaminifu kwa kuwa ameiishi imani yake kishujaa na sasa Kanisa linaingia katika mchakato wa kuhakiki kama mtumishi yule mwaminifu ameshahesabiwa haki kama ni mtakatifu.


Si jambo la ajabu kwamba maana hii au  hatua za utakatifu ni ngeni machoni mwa Watanzania wengi lakini hii inatokana na jambo moja kwamba, katika miaka hamsini ya uhuru, tumekuwa na mtumishi wa Mungu mmoja tu- Mwl. Nyerere, Julius Kambarage na hivyo wengi kuona kama ni ishu ngeni kidogo.
Kuna ngazi kuu tatu ambazo mtu anapitia ili awe mtakatifu, lakini mimi napenda kuziweka nne.
1. Maisha ya uaminifu na ushujaa wa imani.
Mtu anapokuwa anaeuishi ukristu wake kiaminifu anakuwa na nafasi nzuri ya kuishuhudia imani yake kishujaa. Watu wengi watavutiwa na upendo wake kwa Mungu na kwa jirani na kwamba wao wenyewe watakuwa mashuhuda wa kwanza wa matendo ya Mungu kupitia watu hawa mashujaa. Kuuishi ukristu kiaminifu, hauhitaji kufanya miujiza ya kufufua wafu au kuponya wagonjwa, lakini matendo madogo lakini ya upendo mkubwa ni bora zaidi. Hivyo basi, kabla hata taratibu za kikanisa hazijaanza kufatwa, watu wengi watafanya private devotions kwa mashujaa wale.
2. Kutangazwa mtumishi wa Mungu.
Sasa baada ya Kanisa kuona zile private devotions zinavyotia kasi na kwa jinsi ambavyo waumini wanakuzwa imani yao kwa matendo ya Mungu kimwili na kiroho kupitia mtumishi huyu, basi watajibidiisha ili kuchunguza kinachoendelea na wakishajiridhisha, basi wataanza mchakato wa kumtangaza mtakatifu. Hivyo basi watatuma maombi Vatikani na baada ya Vatikani kuridhika basi nao watatoa ruhusa kwamba mchakato uanze napublic devotions ziruhusiwe. Hapo Askofu muhusika wa mahalia atawatangazia waumini na wanachi kwa ujumla akitoa tangazo laitakalotangazwa kwa kipindi cha miezi sita. Tangazo hilo litalenga kuwapa waumini taarifa lakini pia kuwaruhusu kuomba Mungu kupitia maombi ya mtumishi huyo wa Mungu. Atawataka kwamba watakapojibiwa ombi lolote basi wawasiliane na kamati maalumu au kiongozi maalumu wa mchakato huo (postulator).Pia kama kuna mtu anacho kitu chochote cha mtumishi huyo mf. Barua nk. Inabidi pia awasiliane na wahusika aidha kuipeleka nakala halisi au kivuli cha waraka huo.


3. Kutangazwa Mwenyeheri.
Sasa kanisa linahitaji muujiza mmoja ili kumtangaza mtumishi wa Mungu kuwa mtakatifu. Uongo pembeni, hatua hii ni ngumu sana kwani inaweza kuwa ni ya muda mrefu hata karne wa karne. Lakini Mungu huwa na makusudi makuu nay a ajabu sana kwani huwainua watumishi wake pale anapoona ni wakati mwafaka kufanya hivyo kulingana na mahitaji ya kanisa na waumini kwa kipindi kile. Hivyo huwanyanyua watumishi hao kwa malengo tofauti tofauti. Sasa kama ni ugonjwa ndio umepona kutokana na maombi ya mtumishi huyo wa Mungu, basi muujiza huo inabidi uthibitishwe kwamba hakuna science wala nguvu yeyote ya kibinaadamu itakayoweza kuuelezea ubinadamu huo. Hapo itahitaji kuthibitishwa hata na madaktari au wanasayansi ambao hata hawamuamini Mungu. Sasa ile congregation of the doctrine of the cause of saints itamfikishia baba mtakatifu findings zao lakini hata hivyo ni baba mtakatifu pekee ndie mwenye mamlaka baada ya sala kumtangaza mtu kuwa ni mwenye heri.

4. Kutangazwa mtakatifu
Hatua hii ndio kigongo cha vyote kwani mtu anapotangazwa mtakatifu, anakuwa sio tu amenyanyuliwa katika madhabahu ya kanisa lakini pia kitabu cha haki mbinguni. Lakini hii pia ni hatua ngumu sana lakini kila Mungu humpa kila mmoja style ya kipekee.Kwahiyo ukipatikana tena muujiza mwingine basi mwenyeheri basi baba Mtakatifu humtangaza huyo mwenye heri kuwa ni mtakatifu.
Pamoja na ufahamu mdogo wa michakato hii,vilevile huchukua muda  mirefu na huwa inakuwa na gharama nyingi lakini kwa uweza wa Mungu hata wale waiotoka katika maeneo duni kabisa, Mungu huwanyanyua katika madhabahu yake kulingana na mapenzi yake.

Tanzania na watakatifu.
Ingawa ninaamini kabisa watakuwepo watanzania wengi tu mbinguni, lakini hakuna ambaye ameshatangazwa hivyo hata sasa. Lakini mapenzi ya Mungu yana nyakati zake na hivyo alimnyanyua Ml. Nyerere miaka ya hivi karibuni kuwa ni mtumishi wa Mungu, na sasa amemnyanyua sista wa kibenediktini kutoka Peramiho.
Kwakuwa mchakato huu umeanza, nitawaletea mfululizo wa matukio mbalimbali kuhusiana na mtakatifu huyu. Hapo ndipo mtakapomjua Sr. Bernadetha Mbawala ni nani na aliishi vipi imani yake Katoliki.

Isubiri sehemu ya pili ya mfululizo huu wa kumuhusu Sr. Bernadetha OSB.
Ndani ya upendo wa Kristu,
Vicenza-Marie of the Eucharist!