SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Wednesday, September 4, 2013

September 7, a Day of fast and prayer for SYRIA and the World.

The ever smile Pope Francis?




Not today.


He is soooooooooooo sad for whatever is going on in Syria and other parts of the world.


Lets join him on his cause for peace.


"May Peace reign on earth"





I hope we will all join our hands together.


Venerable Bernadetha Mbawala , Pray 4 us



VM

MAENDELEO YA BLOGU YETU

Dear Friends, kwakuwa mchakato wa Mtumishi wa Mungu Bernadetha Mbawala umehamia katika sura mpya ya Kimataifa, wote tunabaki katika sala kuendelea kuuombea mchakato huu hadi hapo tutakaposikia lolote kuhusiana na maendeleo ya mchakato huu.

Nawahimiza mumuombe mtumishi huyu katika mambo mbalimbali na hasa amani ya Tanzania, Afrika ya Mashariki, Syria na dunia nzima kwa ujumla kwani akiwa bad hai, Bernadetha aliiombea sana Urusi ya kipindi kile cha Ukomunisti.
 Hawa ni wakristu waliouawa kwa mabomu kule Arusha wakati wa ufunguzi wa kanisa. Tuwaombee na wao pia watatuombea.

Tuzidi kuomba amani.


Tunawatakia amani wote.

Sunday, December 9, 2012

MCHAKATO WA KUMTANGAZA SR.BERNADETA MBAWALA KUWA MWENYEHERI, WAFIKA UKINGONI

Hayawi hayawi hatimae yanatarajiwa kuwa!
Ule mchakato wa kumtangaza Sr. Bernadetha Mbawala  kuwa mwenyeheri unatarajiwa kufungwa tarehe 14 January, 2013 ikiwa ni miezi kumi tu badala ya miaka miwili kama ilivyo ada.

Habari hii njema ilitolewa na mwakilishi wa Baba Mtakatifu- Benedicto  XVI  Braza Cruz aliyefika nchini hivi karibuni kuja kutathimini mchakato mzima.

Kwa kawaida mchakato wa kumtangaza Mtumishi wa Mungu kuwa Mwenyeheri, una ngazi kuu mbili; Mosi ni ngazi ya jimbo na pili ni ngazi kuu ya Vatikano. Ngazi ya jimbo kwa mfano watoa shuhuda zinazokubalika hutakiwa kuwa 30 lakini kwa sista Bernadeta wamefika 52.

"Nimeridhika na kazi nzuri ambayo imefanyika katika kumtangaza sista Bernadeta Mbawala katika ngazi ya jimbo" alisema Braza Cruz.

Ingawa mchakato umefikia hatua nzuri kijimbo, hatua ya pili ni kubwa sana na gharama ni kubwa. Tunawasihi marafiki wote wa Sr. Bernadeta kuendelea kumuomba Mungu kupitia maombezi yake na mpeleke shuhuda zenu katika kamati ya mchakato jimbo kuu la Songea. Pia tunawahimiza kuendelea kuchangia mchakato huu kifedha kwa kutumia akaunti iliyowekwa hapa kwenye blogu au kwa kuwasiliana na mkuu wa kamati ya fedha Fr. Francis Shawa 0769 845995




Taarifa hii imeletwa na Albano Midelo-
Kamati ya habari, mchakato wa Sr. Bernadeta

Tuesday, June 26, 2012

SALA KUPITIA MAOMBI YA MTUMISHI WA MUNGU Sr. Bernadeta Mbawala


Mchakato wa safari ya Sr. Bernadeta OSB kuelekea uenyeheri bado unaendelea.Natumaini marafiki wenzangu mnamwomba Mungu kupitia maombezi ya sista huyu ili Mungu aweze kutukuzwa kwa kumnyanyua madhabahuni. Yawezekana nduguyo au rafikiyo au jiraniyo au mtu  mwingine anashida kubwa basi tumkimbilie Mungu kupitia Sr. Bernadeta. Wengi wetu wamejibiwa basi tumtukuze Mungu kwa kushirikishana baraka hizo. 

Kama umepewa msaada wowote kupitia maombezi ya Sr. Bernadeta Mbawala, tafadhali toa taarifa kwa Mahakama ya Mchakato, S.L.P 152 Songea, Tanzania Simu 0752253589 au kwa barua pepe mgayajose@yahoo.com 

Monday, May 28, 2012

KITABU KUHUSU MAISHA YA SR. BERNADETA SASA KINAPATIKANA DAR

Kristo!

Wengi walikuwa kiulizia upatikanaji wa kitabu kuhusu maisha ya Sr. Bernadeta Mbawala. Napenda kuwajulisha kwamba kitabu hiko sasa kinapatikana hapa Dar. Acha email yako hapa kwenye comments kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kukipata.
Sr. Bernadeta Mbawala mwandishi ni Pd. Heribert Meyer

MTOTO ALIYEPATIKANA MWA MAOMBEZI YA SR. BERNADETA MBAWALA

Kristu!

Amani na salama kwenu!.

Ingawa wapo watu ambao wameanza kumfahamu Sr Bernadeta hivi karibuni, ukweli ni kwamba Sr. Bermadeta alianza kufahamika hata kabla hajafariki akiwa ni Sr. mgonjwa tena ambaye si msomi. Utakatifu wa Sr. huyu mnyenyekevu ulionekana toka siku hizo. Hii nitaeleza katika maandihi yajayo nikimnukuu Pd. Meyer ambae amemuandika sana Sr. Bernadeta Mbawala.

Sasa baada ya kifo chake, waumini wengi walimiminika katika kaburi la Sr.m Bernadeta wakiomba maombezi yake kwa Mungu. Ni mengi yamesimuliwa, shuhuda nyingi tamutamu zimetolewa na sasa miujiza mingi zaidi inazidi kutendeka katika kaburi hilo.

Sr.Veronika Tiamalis aliyepatikana kwa maombezi ya Sr. Bernadeta akiwa na mama yake
Leo tuangalie shuhuda ya Mama Veronika ambae hakuweza kupata mtoto na hivyo alimkimbnilia Sr. Bernadeta amuombee ili apate mtoto. Basi mama huyu alisikiwa na Mungu akamjalia mtoto kwa kupitia maombezi ya Sr. Bernadeta. Naye mtoto huyo si mweingine bali ni Sr. Veronika Timalias wa shirika la wabenediktini wa Tutzing Pramiho - Songea.

Nawahimiza wasomaji wote kumkimbilia Sr. Bernadeta katika shida zenu mbalimbali na hasa nawahimiza wanawake wenye matatizo ya uzazi.

Iwapo Mungu atakujalia neema yeyote kupitia maombezi ya Sr Bernadeta basi usisite kutoa taarifa.

Monday, May 21, 2012

JOB OPPORTUNITY: WORK WITH EVIDENCE FOR ACTION

Evidence for Action is currently recruiting for two positions: Country Director and Evidence Advisor. 

E4A is a new five-year programme funded by the UK Department for International Development to improve maternal and newborn survival through a combined focus on evidence, advocacy and accountability across six African countries.  

FOR JOB DESCRIPTION and APPLICATION :  Leave your Email address here and we will email you the details.