Hayawi hayawi hatimae yanatarajiwa kuwa!
Ule mchakato wa
kumtangaza Sr. Bernadetha Mbawala kuwa mwenyeheri unatarajiwa kufungwa
tarehe 14 January, 2013 ikiwa ni miezi kumi tu badala ya miaka miwili
kama ilivyo ada.
Habari hii njema ilitolewa na
mwakilishi wa Baba Mtakatifu- Benedicto XVI Braza Cruz aliyefika
nchini hivi karibuni kuja kutathimini mchakato mzima.
Kwa
kawaida mchakato wa kumtangaza Mtumishi wa Mungu kuwa Mwenyeheri, una
ngazi kuu mbili; Mosi ni ngazi ya jimbo na pili ni ngazi kuu ya
Vatikano. Ngazi ya jimbo kwa mfano watoa shuhuda zinazokubalika hutakiwa
kuwa 30 lakini kwa sista Bernadeta wamefika 52.
"Nimeridhika
na kazi nzuri ambayo imefanyika katika kumtangaza sista Bernadeta
Mbawala katika ngazi ya jimbo" alisema Braza Cruz.
Ingawa
mchakato umefikia hatua nzuri kijimbo, hatua ya pili ni kubwa sana na
gharama ni kubwa. Tunawasihi marafiki wote wa Sr. Bernadeta kuendelea
kumuomba Mungu kupitia maombezi yake na mpeleke shuhuda zenu katika
kamati ya mchakato jimbo kuu la Songea. Pia tunawahimiza kuendelea
kuchangia mchakato huu kifedha kwa kutumia akaunti iliyowekwa hapa
kwenye blogu au kwa kuwasiliana na mkuu wa kamati ya fedha Fr. Francis
Shawa 0769 845995
Taarifa hii imeletwa na Albano Midelo-
Kamati ya habari, mchakato wa Sr. Bernadeta
This blog is about the life of a Benedictine nun of St Agnes Chipole-Songea Tanzania who is on her way to sainthood.The blog supports the cause for her beatification by defusing the information so that the faithful can ask for her intercession and offer their moral and financial support to the Archdiocese of Songea to effect the process
SR BERNADETA FUND
Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND
Sunday, December 9, 2012
Tuesday, June 26, 2012
SALA KUPITIA MAOMBI YA MTUMISHI WA MUNGU Sr. Bernadeta Mbawala
Mchakato wa safari ya Sr. Bernadeta OSB kuelekea uenyeheri bado unaendelea.Natumaini marafiki wenzangu mnamwomba Mungu kupitia maombezi ya sista huyu ili Mungu aweze kutukuzwa kwa kumnyanyua madhabahuni. Yawezekana nduguyo au rafikiyo au jiraniyo au mtu mwingine anashida kubwa basi tumkimbilie Mungu kupitia Sr. Bernadeta. Wengi wetu wamejibiwa basi tumtukuze Mungu kwa kushirikishana baraka hizo.
Kama umepewa msaada wowote kupitia maombezi ya Sr. Bernadeta Mbawala, tafadhali toa taarifa kwa Mahakama ya Mchakato, S.L.P 152 Songea, Tanzania Simu 0752253589 au kwa barua pepe mgayajose@yahoo.com
Monday, May 28, 2012
KITABU KUHUSU MAISHA YA SR. BERNADETA SASA KINAPATIKANA DAR
MTOTO ALIYEPATIKANA MWA MAOMBEZI YA SR. BERNADETA MBAWALA
Kristu!
Iwapo Mungu atakujalia neema yeyote kupitia maombezi ya Sr Bernadeta basi usisite kutoa taarifa.
Amani na salama kwenu!.
Ingawa wapo watu ambao wameanza kumfahamu Sr Bernadeta hivi karibuni, ukweli ni kwamba Sr. Bermadeta alianza kufahamika hata kabla hajafariki akiwa ni Sr. mgonjwa tena ambaye si msomi. Utakatifu wa Sr. huyu mnyenyekevu ulionekana toka siku hizo. Hii nitaeleza katika maandihi yajayo nikimnukuu Pd. Meyer ambae amemuandika sana Sr. Bernadeta Mbawala.
Sasa baada ya kifo chake, waumini wengi walimiminika katika kaburi la Sr.m Bernadeta wakiomba maombezi yake kwa Mungu. Ni mengi yamesimuliwa, shuhuda nyingi tamutamu zimetolewa na sasa miujiza mingi zaidi inazidi kutendeka katika kaburi hilo.
Sr.Veronika Tiamalis aliyepatikana kwa maombezi ya Sr. Bernadeta akiwa na mama yake |
Leo tuangalie shuhuda ya Mama Veronika ambae hakuweza kupata mtoto na hivyo alimkimbnilia Sr. Bernadeta amuombee ili apate mtoto. Basi mama huyu alisikiwa na Mungu akamjalia mtoto kwa kupitia maombezi ya Sr. Bernadeta. Naye mtoto huyo si mweingine bali ni Sr. Veronika Timalias wa shirika la wabenediktini wa Tutzing Pramiho - Songea.
Nawahimiza wasomaji wote kumkimbilia Sr. Bernadeta katika shida zenu mbalimbali na hasa nawahimiza wanawake wenye matatizo ya uzazi.
Iwapo Mungu atakujalia neema yeyote kupitia maombezi ya Sr Bernadeta basi usisite kutoa taarifa.
Monday, May 21, 2012
JOB OPPORTUNITY: WORK WITH EVIDENCE FOR ACTION
Evidence for Action is currently recruiting for two positions: Country Director and Evidence Advisor.
E4A is a new five-year programme funded by the UK Department for International Development to improve maternal and newborn survival through a combined focus on evidence, advocacy and accountability across six African countries.
FOR JOB DESCRIPTION and APPLICATION : Leave your Email address here and we will email you the details.
Tuesday, April 24, 2012
SHUHUDA
Je umeshawahi kusaidiwa shida yeyote kama ugonjwa, masomo, kazi n.k? kupitia maombi ya Sr. Bernadeta Mbawala? unaweza kushare nasi? Please do!
Vicenza-Marie
Vicenza-Marie
Monday, April 23, 2012
MASALIA YA MWILI WA SR BERNADETA YAPATIKANA
Maaskofu wa majimbo nane ya metropolitani ya Songea wakishuhudia ufukuaji wa mwili wa Sr Bernadeta Mbawala |
Mwili wa Sr Bernadeta ulifunguliwa mnamo tarehe 24 January, 2012 mbele ya maaskofu wa metropolitani ya Songea ambayo inahusisha majimbo nane ambayo ni Songea, Njombe, Mbinga, Mbeya, Iringa,Tunduru Masasi,Lindi na Mtwara.
Siku ya ufukuzi wa Kaburi hilo watu wengi walivutika kuja kuona kilichomo kani moja, mni jambo geni lakini pili wengi walipatwa na shahuku ya kujua nini kinaweza kitakachoweza kupaatikana kwa mtu aliyekufa miaka hamsini(50) iliyopita.
Sr Bernadeta akinyanyuliwa kuelekea madhabahu ya bwana, kabuli li tupu sasa |
“Mwanzoni tulidhani hakutakuwa na kitu baada ya kukuta mchwa wengi lakini tulipochimba zaidi tlishangaa kuiona mifupa yake, punje za rozari na msalaba” Alisema Fr Francis Shawa ambaye yuko kwenye kamati ya mchakato huu.
Kwa sasa masalia hayo yamehifadhiwa katika kikanisa cha Askofu Mkuu mwashamu Norbert Mtega wa jimbo kuu katoliki la Songea. Kwa sasa utaratibu unaofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Songea wa kujenga mahali rasmi ili kuweka masalia ndani ya Kanisa.
Mifupa na msalaba pia vilipatikana |
Maaskofu wakishuhudia masalia ya Sr. Bernadeta |
Ukiwa umehifadhiwa katika jeneza, mwili wa Sr. Bernadeta ukiingizwa katika kanisa kuu la Mt. Matias Mulumba- Songea |
Hivi karibuni rafiki Vicenza-Marie alipata nafasi ya kuongea na Baba Askofu Norbert Mtega Kurasini Dar eslaam na katika maongezi hayo baba pia aliongelea swala la uhifadhi wa masalia. “Itapasa pia masalia ya Mtumishi wa Mungu yaliyoko Chipole yajengewe mahali maalum pa kuyaweka ndani ya Kanisa, kwani ni muhimu na ni lazima kisheria kufanya hivyo ili kutoa fursa kwa waamini na watu wengine kusali mbele ya Masalia ya Mtumishi wa Mungu na kufanya hija yao huko”
Katika madhabahu ya bwana |
Vilevile baba alisema ya kwamba “Pamoja na sehemu hizo mbili yalipohifadhiwa masalia hayo, itabidi tutengeneze upya kaburi lake pale Peramiho, ili hapo pia pawe ni mahali maalum pa hija kwa watu binafsi wanaotaka kuhiji. Hivyo, hija zitaweza kufanyika: Songea, Chipole, Peramiho na Luwawazi-Likuyufusi, mahali alipozaliwa,”
Saturday, April 21, 2012
Sr Bernadeta Mbawala; Badiliko la jina la blogu
Dear Marafiki,
Kwakuwa blogu hii imeamua kutoa sapoti kwa mchakato wa Sr Bernadeta basi tumeona vyema tukibadili na jina ila kuwarahisishia watafutaji wa blogu hii.
Asanteni sana
Vicenza-Marie
Kwakuwa blogu hii imeamua kutoa sapoti kwa mchakato wa Sr Bernadeta basi tumeona vyema tukibadili na jina ila kuwarahisishia watafutaji wa blogu hii.
Asanteni sana
Vicenza-Marie
Friday, April 20, 2012
MAPENZI MAKUU KWA MAMA BIKIRA MARIA
Dear Marafiki
Sr Bernadeta akisali katika kipango (Grotto) ya mama Bikira Maria, Peramiho. |
Leo tunaangalia kwa kifupi uhusiano wa watakatifu; wao kwa wao. Unadhani kitu gani wanashabihiana? Katika kupitia vitabu mbalimbali vya maisha ya watakatifu, nimegundua vitu vingi ambavyo wanashabihiana. Mfano wa maeneo/ viyu hivyo ni pamoja na Mapenzi yao na imani thabiti kwa Ekaristi takatifu,imani kwa mama Bikira Maria na mateso;kuyapenda na kuyavumilia kwa saburi wakiyatolea kwa nia mbalimbali.
Sr Bernadeta alikuwa na mapenzi makubwa kwayo pia. Mapenzi kwa Ekaristi na kwa mama Bikira Maria
Sr Bernadeta Mbawala;tumuombe, tumtangaze, kwa sifa na utukufu wa Mungu!
Vicenza-Marie!
Subscribe to:
Posts (Atom)