SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Tuesday, February 14, 2012

SIKUKUU YA MTAKATIFU VALENTINO-PADRE NA MFIA DINI

Valentine alikuwa ni Padre mtakatifu kule Roma ambae yeye, Mt Marius na familia yake waliwasaidia wafia dini wakati wa utawala ule dhalimu wa Cledius wa pili.Alikamatwa na kupelekwa Roma ambae alimlazimisha kuikana imani yake. Walakini alipoona Valentine haikani, basi aliamuru apigwe kwa magongona baadae achinjwe.Hivyo basi alichinjwa tarehe 14 Februari, 270. Inasemekana kwamba Papa Julius wa kwanza alijenga kanisa Ponte Mole kwa heshima ya Valentini kwa muda mrefu kuna gati inaitwa Porta del Popolo au zamani Porta Valetin.

Sehemu kubwa ya masalia yake yapo katikakanisa la Mt. Praxeda

Inaaminika kwamba wakati ule wa udhalimu wa ukristu, Mt. Valentino aliwafungisha ndoa za siri watu wengi na hivyo kuhusianishwa sana na swala zima la upendo,

Nawatakieni sikukuu njema ya wapendanao.

Nami nawapenda sana

Vicenza-Marie!

Thursday, February 2, 2012

SIKUKUU YA MTAKATIFU BLAS;ASKOFU NA MFIA DINI

Namshukuru Mungu kwakuwa shingo yangu na koo langu vimebarikiwa katika sikukuu hii ya Mt. Blas.

Mungu na atusaidie tuweze kuitetea imani yetu hata iibidi kumwaga damu kwaajiliyo.

Vicenza-marie

SHEREHE YA YESU KUTOLEWA HEKALUNI

SHEREHE YA YESU KUTOLEWA HEKALUNI

Fahamu Kanisa Katoliki na Kanisa la kiorthodoksi: Makutano na maachano


Yesu Kristu alianzishakanisa kanisa moja tu na kuliacha mikononi mwa mtume Petro. Sasa baada ya Kristu kupaa, mitume hasa Petro na Paulo walienda Roma kwakuwa pale ndipo palikuwa ni kiini cha ustaarabu kwani Ili mambo yaende, ilibidi kufanya toka Rumi. Mwanzoni wakristu walipata shida sana kule Roma na ndio maana leo tunao mashahidi wa Roma ambao walisingiziwa na mfalme Nero kwamba waliuchoma mji wa Roma kumbe inasadikiwa ni Nero mwenyewe aliuchoma mji ule.
Sasa ilipofikwa mwaka313BK Mfalme Contatine mtoto wa Mt. Helena aliruhusu Ukristu na baadae kuufanya kuwa ndiyo dini ya Roma. Baadae Mfalme aliamua kuhamishia himaya yake Constatinopole  (Uturuki ya sasa) na makao makuu ya kanisa yakawa yamebaki kule Roma. Lakini ilipofika miaka ya 476BK, Himaya ya Rumi ilianguka na hivyo basi Roma pia ilipoteza ule umaarufu wake wa kuwa ndicho kiini cha ustaarabu duniani. Wale wa masharikI ambao ndio Waorthodoksi wa sasa wakabaki huko constatinopole na ugiriki n.k na wakawa wanatumia kigiriki wakati wale wa Mashariki waliendelea na Kilatini.
Waothordoxy wakakataa mamlaka ya Papa na pia wakakataa kusema kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa baba na mwana wao wanasema anatoka kwa baba tu.
Kimsingi, kunatofauti ndogondogo katika theolojia yetu lakini vingi sana tunafanana.
Natumaini wengine watachangia zaidi.