SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Tuesday, April 24, 2012

SHUHUDA

Je umeshawahi kusaidiwa shida yeyote kama ugonjwa, masomo, kazi n.k? kupitia maombi ya Sr. Bernadeta Mbawala? unaweza kushare nasi? Please do!

Vicenza-Marie

Monday, April 23, 2012

MASALIA YA MWILI WA SR BERNADETA YAPATIKANA

Maaskofu wa majimbo nane ya metropolitani ya Songea wakishuhudia ufukuaji wa mwili wa Sr Bernadeta Mbawala




Mwili wa Sr Bernadeta ulifunguliwa mnamo tarehe 24 January, 2012 mbele ya maaskofu wa metropolitani ya Songea ambayo inahusisha majimbo  nane ambayo ni Songea, Njombe, Mbinga, Mbeya, Iringa,Tunduru Masasi,Lindi na Mtwara.


Siku ya ufukuzi wa Kaburi hilo watu wengi walivutika kuja kuona kilichomo kani moja, mni jambo geni lakini pili wengi walipatwa na shahuku ya kujua nini kinaweza kitakachoweza kupaatikana kwa mtu aliyekufa miaka hamsini(50) iliyopita.
Sr Bernadeta akinyanyuliwa kuelekea madhabahu ya bwana, kabuli li tupu sasa     
“Mwanzoni tulidhani hakutakuwa na kitu baada ya kukuta mchwa wengi lakini tulipochimba zaidi tlishangaa kuiona mifupa yake, punje za rozari na msalaba” Alisema Fr Francis Shawa ambaye yuko kwenye kamati ya mchakato huu.

Kwa sasa masalia hayo yamehifadhiwa katika kikanisa cha Askofu Mkuu mwashamu Norbert Mtega wa jimbo kuu katoliki la Songea. Kwa sasa utaratibu unaofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Songea wa kujenga mahali rasmi ili kuweka masalia ndani ya Kanisa.
Mifupa na msalaba pia vilipatikana




Maaskofu wakishuhudia masalia ya Sr. Bernadeta
Ukiwa umehifadhiwa katika jeneza, mwili wa Sr. Bernadeta ukiingizwa katika kanisa kuu la Mt. Matias Mulumba- Songea
Hivi karibuni rafiki Vicenza-Marie alipata nafasi ya kuongea na Baba Askofu Norbert Mtega Kurasini Dar eslaam na katika maongezi hayo baba pia aliongelea swala la uhifadhi wa masalia. “Itapasa pia masalia ya Mtumishi wa Mungu yaliyoko Chipole yajengewe mahali maalum pa kuyaweka ndani ya Kanisa, kwani ni muhimu na ni lazima kisheria kufanya hivyo ili kutoa fursa kwa waamini na watu wengine kusali mbele ya Masalia ya Mtumishi wa Mungu na kufanya hija yao huko”
Katika madhabahu ya bwana
Vilevile baba alisema ya kwamba  “Pamoja na sehemu hizo mbili yalipohifadhiwa masalia hayo, itabidi tutengeneze upya kaburi lake pale Peramiho, ili hapo pia pawe ni mahali maalum pa hija kwa watu binafsi wanaotaka kuhiji. Hivyo, hija zitaweza kufanyika: Songea, Chipole, Peramiho na Luwawazi-Likuyufusi, mahali alipozaliwa,” 
Shime shime marafiki pelekeni shida zenu;magonjwa, masomo,matatizo ya uzazi na kadhalika kwa Mungu kupitia maombezi ya sista huyu ili aweze kuingia katika orodha ya watakatifu. Pia tunaomba kuchangia mchakato huu kwa akaunti ya jimbo la Songea ili kufanikisha mchakato huu ambao nighali sana.

Katika upendo wa Kristu,

Vicenza-Marie

Saturday, April 21, 2012

Sr Bernadeta Mbawala; Badiliko la jina la blogu

Dear Marafiki,

Kwakuwa blogu hii imeamua kutoa sapoti kwa mchakato wa Sr Bernadeta basi tumeona vyema tukibadili na jina ila kuwarahisishia watafutaji wa blogu hii.

Asanteni sana

Vicenza-Marie

Friday, April 20, 2012

MAPENZI MAKUU KWA MAMA BIKIRA MARIA

Dear Marafiki

Sr Bernadeta akisali katika kipango (Grotto) ya mama Bikira Maria, Peramiho.
Leo tunaangalia kwa kifupi uhusiano wa watakatifu; wao kwa wao. Unadhani kitu gani wanashabihiana? Katika kupitia vitabu mbalimbali vya maisha ya watakatifu, nimegundua vitu vingi ambavyo wanashabihiana. Mfano wa maeneo/ viyu hivyo ni pamoja na Mapenzi yao na imani thabiti kwa Ekaristi takatifu,imani kwa mama Bikira Maria na mateso;kuyapenda na kuyavumilia kwa saburi wakiyatolea kwa nia mbalimbali.

Sr Bernadeta alikuwa na mapenzi makubwa kwayo pia. Mapenzi kwa Ekaristi na kwa mama Bikira Maria




Sr Bernadeta Mbawala;tumuombe, tumtangaze, kwa sifa na utukufu wa Mungu!


Vicenza-Marie!

Thursday, April 19, 2012

MAISHA YA SR BERNADETA: NYOTA YENYE KUSISIMUA

Sr Bernadeta Mbawala (Akiitwa Klara kabla ya kuingia utawa)
Picha kwa hisani ya Pd. Herbert Meyer!

CHANGIA MCHAKATO WA Sr. BENADETA KUPITIA MFUKO WA BENADETA WA JIMBO KUU KATOLIKI SONGEA


Mchakato wa safari ya uenye heri ya rafiki yetu Sr Benadeta Mbawala ni ghali mno. Tunaombwa kumuongezea Mwashamu baba Askofu Mkuu Norbet Mtega nguvu. Wameanzisha mfuko pale jimboni kupitia Bank ya CRDB: 

 Sr Bernadeta Fund, CRDB Bank, Account number.        0152085128521



Chonde Chonde


"Sr Benadeta Mbawala: Tumtangaze, Tumuombe kwa sifa na utukufu wa Mungu"



 Vicenza- Marie