SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Wednesday, November 23, 2011

Katekisimu Klass

Darasa la watoto wakatekisimu

Dear Marafiki


Alice, Erick and Vicenza- marie wameamua kuwafundisha watoto Katekisimu ya kanisa katoliki.
Sote watatu ni vijana wa jumuiya ya Mt. Francisco wa Asizi, Parokia ya Maria Mtakatifu Kimara Mwisho. Parokia yetu iko barabara ya Morogoro na wote wapitao hapo aidha wakiwa wanaenda au wanatoka mikoani ni lazima wapite hapo. Basi toka ukiwa mbali utaona minara mirefu na paa la kanisa letu zuri. Ingawa parokia yetu inamiaka mitano tu, imekuwa sana sana kutokana na maombezi ya msimamizi wetu mama Maria Mtakatifu, mapadri wetu waklareti (Claretian Fathers) pamoja na waumini wote.

Katika Parokia yetu pia huwa tunaabudu Ekaristi takatifu kwa kukesha kila ijumaa ya kwanza ya mwezi. Pia kila siku milango huwa wazi hadi saa mbili au tatu usiku ili watu waweze kuendesha sala zao binafsi.

Pia tuna grotto kubwa sana ya mama Maria na kwa sasa tunajenga nyumba ya mapadri. Well, kibali kitatoka ndani ya wiki mbili lakini michango bado inaendelea.


Back to Katekisimu klass, basi sisi vijana  watatu wa parokia tuliona ni vyema kama tungewafundisha wadogo zetu imani yetu Katoliki ili waweze kukua vyema kama Yesu mwenyewe.

Kiukweli tunaona ni baraka ya pekee kuvifundisha vitoto hivi katekisimu. Vinafurahi kweli hata sisi tunapata furaha kubwa sana moyoni.
Mmoja wa walimu wa Katekisimu Alice Mchomvu akiwasikiliza watoto


Masomo hayo hufundishwa kila siku ya jumamosi mara tu baada ya jumuiya. Watoto hukusanyika nyumbani kwa Vicenza-marie ambako hufundishwa kisha hupata chai.

Wanajifunza yafuatayo

1. Katekisimu ya kanisa katoliki
2. biblia
3.Maisha ya watakatifu (Pia huangalia sinema mbalimbali za maisha ya watakatifu zilizo katika katuni)
4. Huchora vitu mbalimbali vya kwenye biblia
5. kuimba na
6. Kujifunza nyimbo mbalimbali.
Watoto wa darasa la Katekisimu wakijiandaa kuangalia filamu ya maisha ya Mt. Francisco wa Asizi

Tunapenda kuwahamasisha vijana wengi mjitolee kuwafundisha wadogo zenu imani yenu Katoliki.
"Najivunia ukatoliki wangu"- Angela Kessy


"Kwahiyo, yeyote ambae atawafundisha wengine mambo haya ataitwa mdogo katika ufalme wa Mungu, lakini kwa yeyote atakayeyaishi haya na kuwafundisha wengine ipasavyo ataitwa mkuu katika ufalme wa Mungu"

Ndani ya upendo wa kristu,

Vicenza-Marie of the Eucharist

Monday, November 21, 2011

PROCESSION

Katika jumapili ya mwisho wa mwezi wa kumi, Parokia ya Maria Mtakatifu ilifanya maandamano katika vitongoji vya kimara ili  kusherehekea sikukuu ya bikira maria msimamizi wa parokia yetu na vilevile kufunga mwezi wa rozari. Ilikuwa ni siku kubwa na nzuri sana na kwa miaka mingi (sina uhakika kama ilishafanyika nyuma) Parokia ya Kimara ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya maandamano hayo ya aina yake.

Baba Paroko alianza kwa kuibariki sanamu ya bikira Maria kabla ya WAWATA hawajaibeba kwenda nayo nje tayari kwa maandamano.
 (Baba Paroko akijiandaaa na kuibariki sanamu ya Bikira Maria)

Nami nilimfwata mwenyekiti wa Liturujia nikiomba ruhusa ya kufotoa, akakubali.
 Paroko anabariki sanamu ya Mama Maria


Baada ya baraka, ndipo WAWATAwalipoibeba sanamu kwa heshima kuipeleka nje
WAWATA.


Kisha, Mama Bikira Maria alipandishwa katika gari maalumu ambayo pia ilichukua watoto wa utatu mtakatifu, WAWATA na baadhi ya wanakwaya.


Waumini
Maandamano

Sunday, November 13, 2011

Mimi, Parokia yangu na Imani yangu katoliki

Baada ya kuona kwamba mimi na parokia yangu tunavyoweza au tulivyo na wajibu wa kueneza imani katoliki ili kueneza upendo na utukufu wa Mungu, blogu hii inakuja ikiwa na lengo la kuonesha matukio mbalimbali yanayofanywa na parokia yangu ya Maria Mtakatifu iliyoko Kimara katika jimno kuu la Dar es Salaam katika uenezaji wa injili.
Tafadhali safiri na mimi katika safari hii ya kiroho, safari itakayokuinjilisha na kuikuza imani yako katoliki. Nawaalika wote wale wasiyoiaju, wale wasiotaka kuijua, wale wasioaiamini na wakatoliki wenzangu ili tupate kuijua imani katoliki inayoongozwa na kanisa lilioanzishwa na Kristu mwenyewe.

Karibuni,

Vicenza-marie