SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Sunday, March 25, 2012

SALA KWA MTUMISHI WA MUNGU SR BERNADETHA

Marafiki wapendwa,

Kuna ombi maalumu nimepewa na rafiki mmoja naomba tumuombee katika shida yake hiyo. Mmkumbuke katika sala na hasa tukiisali sala hii ya kuelekea kumtakatifuza Sr. Bernadetha Mbawala katika madhabahu ya bwana.

Katika kristu,

Vicenza-marie!

Tuesday, March 6, 2012

Sr Bernadetha Mbawala: Updates

Wapendwa rafiki,
Kutokana na mchakato unaoendelea kuhusiana na swala nzima la kumtakatifuza Sr Benadetha Mbawala, shughuli kuu ya blogui hii itakuwa ni kuhusu Sr Mbawala tu. Naiweka na sala yake hapa jamani mwenye ombi lolote (Najua hakuna ambaye hana) basi aisali sala hii na shuhuda zenu mziweke humu ili tuweze kuzifikisha jimboni Songea na ikithibitishwa-kulintgana na sheria za kanisa basi mtyumishi huyu aweze kuwekwa madhabahuni mwa bwana. Karibuni mno.

Ifuatayo ni sala iliyotolewa na jimbo kuu Songea.
SALA KWA MTUMISHI WA MUNGU SR. BENADETHA MBAWALA OSB

Ee baba wa mbinguni, kwa njia ya mtumishi wako Sista Benadetha Mbawala, umelipatia kanisa lako,katika ulimwengu huu uliojaa mateso na magonjwa, ushuhuda mkubwa, juu ya nguvu za ukombozi zipatikanazo kwa msalaba wako mtakatifu. Kwa maombezi ya mtumishi wako, utujalie kwwa wema wako usio na kipimo, tupate yale tunayoomba (TAJA OMBI LAKO).

Tunaomba hayo kwa njia ya Yesu Kristu Bwana wetu. Amina.