SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Sunday, December 9, 2012

MCHAKATO WA KUMTANGAZA SR.BERNADETA MBAWALA KUWA MWENYEHERI, WAFIKA UKINGONI

Hayawi hayawi hatimae yanatarajiwa kuwa!
Ule mchakato wa kumtangaza Sr. Bernadetha Mbawala  kuwa mwenyeheri unatarajiwa kufungwa tarehe 14 January, 2013 ikiwa ni miezi kumi tu badala ya miaka miwili kama ilivyo ada.

Habari hii njema ilitolewa na mwakilishi wa Baba Mtakatifu- Benedicto  XVI  Braza Cruz aliyefika nchini hivi karibuni kuja kutathimini mchakato mzima.

Kwa kawaida mchakato wa kumtangaza Mtumishi wa Mungu kuwa Mwenyeheri, una ngazi kuu mbili; Mosi ni ngazi ya jimbo na pili ni ngazi kuu ya Vatikano. Ngazi ya jimbo kwa mfano watoa shuhuda zinazokubalika hutakiwa kuwa 30 lakini kwa sista Bernadeta wamefika 52.

"Nimeridhika na kazi nzuri ambayo imefanyika katika kumtangaza sista Bernadeta Mbawala katika ngazi ya jimbo" alisema Braza Cruz.

Ingawa mchakato umefikia hatua nzuri kijimbo, hatua ya pili ni kubwa sana na gharama ni kubwa. Tunawasihi marafiki wote wa Sr. Bernadeta kuendelea kumuomba Mungu kupitia maombezi yake na mpeleke shuhuda zenu katika kamati ya mchakato jimbo kuu la Songea. Pia tunawahimiza kuendelea kuchangia mchakato huu kifedha kwa kutumia akaunti iliyowekwa hapa kwenye blogu au kwa kuwasiliana na mkuu wa kamati ya fedha Fr. Francis Shawa 0769 845995




Taarifa hii imeletwa na Albano Midelo-
Kamati ya habari, mchakato wa Sr. Bernadeta