Katika jumapili ya mwisho wa mwezi wa kumi, Parokia ya Maria Mtakatifu ilifanya maandamano katika vitongoji vya kimara ili kusherehekea sikukuu ya bikira maria msimamizi wa parokia yetu na vilevile kufunga mwezi wa rozari. Ilikuwa ni siku kubwa na nzuri sana na kwa miaka mingi (sina uhakika kama ilishafanyika nyuma) Parokia ya Kimara ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya maandamano hayo ya aina yake.
Baba Paroko alianza kwa kuibariki sanamu ya bikira Maria kabla ya WAWATA hawajaibeba kwenda nayo nje tayari kwa maandamano.
(Baba Paroko akijiandaaa na kuibariki sanamu ya Bikira Maria)
Nami nilimfwata mwenyekiti wa Liturujia nikiomba ruhusa ya kufotoa, akakubali.
Paroko anabariki sanamu ya Mama Maria
Baada ya baraka, ndipo WAWATAwalipoibeba sanamu kwa heshima kuipeleka nje
WAWATA.
Kisha, Mama Bikira Maria alipandishwa katika gari maalumu ambayo pia ilichukua watoto wa utatu mtakatifu, WAWATA na baadhi ya wanakwaya.
Waumini
Maandamano
This blog is about the life of a Benedictine nun of St Agnes Chipole-Songea Tanzania who is on her way to sainthood.The blog supports the cause for her beatification by defusing the information so that the faithful can ask for her intercession and offer their moral and financial support to the Archdiocese of Songea to effect the process
SR BERNADETA FUND
Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND
No comments:
Post a Comment
Dear Rafiki,
Asante kwa comments zako
Vicenza-Marie!