SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Tuesday, February 14, 2012

SIKUKUU YA MTAKATIFU VALENTINO-PADRE NA MFIA DINI

Valentine alikuwa ni Padre mtakatifu kule Roma ambae yeye, Mt Marius na familia yake waliwasaidia wafia dini wakati wa utawala ule dhalimu wa Cledius wa pili.Alikamatwa na kupelekwa Roma ambae alimlazimisha kuikana imani yake. Walakini alipoona Valentine haikani, basi aliamuru apigwe kwa magongona baadae achinjwe.Hivyo basi alichinjwa tarehe 14 Februari, 270. Inasemekana kwamba Papa Julius wa kwanza alijenga kanisa Ponte Mole kwa heshima ya Valentini kwa muda mrefu kuna gati inaitwa Porta del Popolo au zamani Porta Valetin.

Sehemu kubwa ya masalia yake yapo katikakanisa la Mt. Praxeda

Inaaminika kwamba wakati ule wa udhalimu wa ukristu, Mt. Valentino aliwafungisha ndoa za siri watu wengi na hivyo kuhusianishwa sana na swala zima la upendo,

Nawatakieni sikukuu njema ya wapendanao.

Nami nawapenda sana

Vicenza-Marie!

No comments:

Post a Comment

Dear Rafiki,
Asante kwa comments zako


Vicenza-Marie!