Yesu Kristu alianzishakanisa kanisa moja tu na kuliacha mikononi mwa mtume Petro. Sasa baada ya Kristu kupaa, mitume hasa Petro na Paulo walienda Roma kwakuwa pale ndipo palikuwa ni kiini cha ustaarabu kwani Ili mambo yaende, ilibidi kufanya toka Rumi. Mwanzoni wakristu walipata shida sana kule Roma na ndio maana leo tunao mashahidi wa Roma ambao walisingiziwa na mfalme Nero kwamba waliuchoma mji wa Roma kumbe inasadikiwa ni Nero mwenyewe aliuchoma mji ule.
Sasa ilipofikwa mwaka313BK Mfalme Contatine mtoto wa Mt. Helena aliruhusu Ukristu na baadae kuufanya kuwa ndiyo dini ya Roma. Baadae Mfalme aliamua kuhamishia himaya yake Constatinopole (Uturuki ya sasa) na makao makuu ya kanisa yakawa yamebaki kule Roma. Lakini ilipofika miaka ya 476BK, Himaya ya Rumi ilianguka na hivyo basi Roma pia ilipoteza ule umaarufu wake wa kuwa ndicho kiini cha ustaarabu duniani. Wale wa masharikI ambao ndio Waorthodoksi wa sasa wakabaki huko constatinopole na ugiriki n.k na wakawa wanatumia kigiriki wakati wale wa Mashariki waliendelea na Kilatini.
Waothordoxy wakakataa mamlaka ya Papa na pia wakakataa kusema kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa baba na mwana wao wanasema anatoka kwa baba tu.
Kimsingi, kunatofauti ndogondogo katika theolojia yetu lakini vingi sana tunafanana.
Natumaini wengine watachangia zaidi.
No comments:
Post a Comment
Dear Rafiki,
Asante kwa comments zako
Vicenza-Marie!