Kutokana na mchakato unaoendelea kuhusiana na swala nzima la kumtakatifuza Sr Benadetha Mbawala, shughuli kuu ya blogui hii itakuwa ni kuhusu Sr Mbawala tu. Naiweka na sala yake hapa jamani mwenye ombi lolote (Najua hakuna ambaye hana) basi aisali sala hii na shuhuda zenu mziweke humu ili tuweze kuzifikisha jimboni Songea na ikithibitishwa-kulintgana na sheria za kanisa basi mtyumishi huyu aweze kuwekwa madhabahuni mwa bwana. Karibuni mno.
Ifuatayo ni sala iliyotolewa na jimbo kuu Songea.
SALA KWA MTUMISHI WA MUNGU SR. BENADETHA MBAWALA OSB
Ee baba wa mbinguni, kwa njia ya mtumishi wako Sista Benadetha Mbawala, umelipatia kanisa lako,katika ulimwengu huu uliojaa mateso na magonjwa, ushuhuda mkubwa, juu ya nguvu za ukombozi zipatikanazo kwa msalaba wako mtakatifu. Kwa maombezi ya mtumishi wako, utujalie kwwa wema wako usio na kipimo, tupate yale tunayoomba (TAJA OMBI LAKO).
Tunaomba hayo kwa njia ya Yesu Kristu Bwana wetu. Amina.
AMINA.....Sr.Bernedetha daima utuombee kwa Mungu ili nna sisi tuweze kufikia makao ya Mungu...utusaidie huku duniani tunapoaangaika
ReplyDeleteSr Bernadeta Mbawala.TUMTANGAZE< TUMUOMBE KWA SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU
ReplyDeletetembelea Link hii pia bonyeza LIKE Asante http://www.facebook.com/BERNADETAMBAWALA
ReplyDeletePia unaweza kutufwata kwenye tweter yetu SrMbawala au bofya follow kwenye kialama cha tweeter hapa kwenye blogu
DeleteVicenza- Marie