SR BERNADETA FUND

Kindly assist the Archidiocese of Songea by contributing to the beatification process of Sr. Bernadeta Mbawala through their CRDB account no. 0152085128521, account name:SR. BERNADETA FUND

Monday, April 23, 2012

MASALIA YA MWILI WA SR BERNADETA YAPATIKANA

Maaskofu wa majimbo nane ya metropolitani ya Songea wakishuhudia ufukuaji wa mwili wa Sr Bernadeta Mbawala




Mwili wa Sr Bernadeta ulifunguliwa mnamo tarehe 24 January, 2012 mbele ya maaskofu wa metropolitani ya Songea ambayo inahusisha majimbo  nane ambayo ni Songea, Njombe, Mbinga, Mbeya, Iringa,Tunduru Masasi,Lindi na Mtwara.


Siku ya ufukuzi wa Kaburi hilo watu wengi walivutika kuja kuona kilichomo kani moja, mni jambo geni lakini pili wengi walipatwa na shahuku ya kujua nini kinaweza kitakachoweza kupaatikana kwa mtu aliyekufa miaka hamsini(50) iliyopita.
Sr Bernadeta akinyanyuliwa kuelekea madhabahu ya bwana, kabuli li tupu sasa     
“Mwanzoni tulidhani hakutakuwa na kitu baada ya kukuta mchwa wengi lakini tulipochimba zaidi tlishangaa kuiona mifupa yake, punje za rozari na msalaba” Alisema Fr Francis Shawa ambaye yuko kwenye kamati ya mchakato huu.

Kwa sasa masalia hayo yamehifadhiwa katika kikanisa cha Askofu Mkuu mwashamu Norbert Mtega wa jimbo kuu katoliki la Songea. Kwa sasa utaratibu unaofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Songea wa kujenga mahali rasmi ili kuweka masalia ndani ya Kanisa.
Mifupa na msalaba pia vilipatikana




Maaskofu wakishuhudia masalia ya Sr. Bernadeta
Ukiwa umehifadhiwa katika jeneza, mwili wa Sr. Bernadeta ukiingizwa katika kanisa kuu la Mt. Matias Mulumba- Songea
Hivi karibuni rafiki Vicenza-Marie alipata nafasi ya kuongea na Baba Askofu Norbert Mtega Kurasini Dar eslaam na katika maongezi hayo baba pia aliongelea swala la uhifadhi wa masalia. “Itapasa pia masalia ya Mtumishi wa Mungu yaliyoko Chipole yajengewe mahali maalum pa kuyaweka ndani ya Kanisa, kwani ni muhimu na ni lazima kisheria kufanya hivyo ili kutoa fursa kwa waamini na watu wengine kusali mbele ya Masalia ya Mtumishi wa Mungu na kufanya hija yao huko”
Katika madhabahu ya bwana
Vilevile baba alisema ya kwamba  “Pamoja na sehemu hizo mbili yalipohifadhiwa masalia hayo, itabidi tutengeneze upya kaburi lake pale Peramiho, ili hapo pia pawe ni mahali maalum pa hija kwa watu binafsi wanaotaka kuhiji. Hivyo, hija zitaweza kufanyika: Songea, Chipole, Peramiho na Luwawazi-Likuyufusi, mahali alipozaliwa,” 
Shime shime marafiki pelekeni shida zenu;magonjwa, masomo,matatizo ya uzazi na kadhalika kwa Mungu kupitia maombezi ya sista huyu ili aweze kuingia katika orodha ya watakatifu. Pia tunaomba kuchangia mchakato huu kwa akaunti ya jimbo la Songea ili kufanikisha mchakato huu ambao nighali sana.

Katika upendo wa Kristu,

Vicenza-Marie

14 comments:

  1. Asante kwa taarifa hii nzuri kwa kweli inatupa hamasa na kutufumbua macho. tuambie taratibu za kuchangia mchakato huu hiyo akaunti ya jimbo ni ipi?

    Naitwa Neema Mbilinyi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dear Neema,
      Asante kwa kutembelea blogu na kwa nia yako njema ya kuchangia. Tumeweka akaunti ya jimbo kuu Songea mahsusi kwa kuchangia mchakato tafadhali isome hapo mwanzo mwa blogu.


      Katika upendo wa Kristu,

      Vicenza- Marie

      Delete
    2. Ninamshukuru mungu kwa kunipa nafasi ya kuona na kushuhudia utakatifu wa mtumishi wake Sr Bernadeta Mbawala of Saint Agnes Chipole. Siku ya kwanza kusikia jina lake i was somehow young i felt the deep click and being aspired to go, sometimes i tried to ignore it, but i found my self one day packed and ready to go there. Ulikuwa wakati wa pekee sana. Kimsingi ni ngumu kueleza lakini tangu nilipokwenda mara ya kwanza sehemu ile, kila nikaribiapo na kufanya sala amani ya pekee moyoni(totally new world), i feel more near by, nikitoka pale ni wepesi wa moyo na salvation. Nikiondoka, ninayo yapata hunistaajabisha na kunifanya nirudi na niliahidi sito acha kwenda mahala pale kwani bwana amenipa nafasi ya pekee sana kupitia mahala pale. Jina la bwana lihimidiwe.

      Delete
  2. Asante kwa kuboresha blog yetu hii,Nazidi kumtangaza mtumishi wa Mungu naamini nitatoa ushuhuda relevant wenye vithibitisho,mzidi kuniombea.
    zacharia Martin

    ReplyDelete
  3. nashukuru kwa kujitoa kwako kutuhabarisha habari ya MTUMISHI WA MUNGU SR.BENEDETHA MBAWALA OSB..........

    ReplyDelete
  4. Ni Jambo jema. tutashirikiana kufanya hilo jambo Mungu aweke baraka tufikie malengo. Amina
    Flaviana Msaki

    ReplyDelete
  5. Ni msimamo na ni heshima kwa kanisa letu,pia ni mwanga kwa kanisa letu,Mungu atusaidie tudumu katika imani daima.tutashirikiana kiroho,kimwili na kiuchumi ilitufanikiwe katika hilo.

    ReplyDelete
  6. Nina imani kwa maombezi ya sista huyu mnyenyekevu Ombi langu la kuiunganisha familia yangu, japo sistahili, litapokelwa na baba yangu wa mbinguni. Naye atanioniea huruma na kunijalia Baraka hii kupitia uongofu wa kweli. Nitaomba mpaka nijibiwe! Amina.

    ReplyDelete
  7. Ni jambo jema, tumuombee mama Bernadeta kwa Mungu,hakika ni heri kumtumikia Mungu tungali hai..ili tudumu ktk Kristo.

    ReplyDelete
  8. Ni jambo jema, tumuombee mama Bernadeta kwa Mungu,hakika ni heri kumtumikia Mungu tungali hai..ili tudumu ktk Kristo.

    ReplyDelete
  9. Mungu ni mwema na mwenye huruma wakati wote... Hakika matendo yake mema yanaonekana duniani ! Tunaomba imani kwa jina lake Baba muumba Wa mbingu na aridhi atuzidishie imani. Amina

    ReplyDelete
  10. Mwenyezi Mungu atuongoze na sisi tutende yale yaliyo mema ya kumpendeza kwa maana Sr.Bernadeta kawa mfano wa kuiga. Muda haujaisha wa kufanya mema, hakika inabidi tujitafakari na pia tuhakikishe tunamtangaza Sr. Bernadeta katika ulimwengu.

    ReplyDelete
  11. Tumsifi Yesu Kristu!
    Naombeni Historia ya Sister Banerdeta

    ReplyDelete
  12. TYK, aksanteni sana Kwa hizi habari njema za Mtumishi wa Mungu Sr Bernadeta. Nina changamoto Mbili ktk maisha yangu na familia, kwa upendo huu tulionao kama familia, nitamshirikisha Sr Bernadette atuombee Kwa Mungu Ili Mama Kania aone nia yetu njema kwa Kanisa na Imani yeti kwake, na pili Mama Betnadeta atuombee Kwa Mungu tuweze kupata matunda ya hiki tulichokipanda kama mbegu maishani.

    ReplyDelete

Dear Rafiki,
Asante kwa comments zako


Vicenza-Marie!